Na Mwandishi Wetu
USHINDI wa Donald Trump wa kurudi tena katika Ikulu ya Marekani, kutaweza kuwa neema kwa mfuasi wake mkubwa Elon Musk.
Tajiri Elon Musk anayeelezwa kuwa ni tajiri mkubwa nchini Marekani alisalia na Trump wakati wa kampeni zake na hata uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba nne, mwaka huu.
Hivyo wadadisi wa siasa wanaeleza kuwa kurudi Ikulu kwa Trump kunaweza kuwa ushindi kwa Musk ambaye hata wakati ambapo matokeo yalitolewa ndiye aliyekuwepo na mgombea huyo.
Hata kwenye hotuba yake, Trump alitumia dakika kadhaa kumsifia rafiki yake huyo.
Musk aliunga mkono chama cha Republican mara tu baada ya jaribio la kumuua Trump huko Butler, Pennsylvania mwezi Julai, mwaka huu.
Akiwa mmoja wa waungaji mkono muhimu wa rais mteule, bilionea huyo wa teknolojia alichangia zaidi ya $119m (£92m) kufadhili kundi la kumuunga mkono Trump Super PAC lililomfanyia kampeni Donald Trump.