MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: PURA Yajipanga Gesi Asilia Itumike Kwenye Magari
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > PURA Yajipanga Gesi Asilia Itumike Kwenye Magari
Habari

PURA Yajipanga Gesi Asilia Itumike Kwenye Magari

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), imesema inajipanga kuhakikisha gesi asilia inatumika pia kwenye magari.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Ushirikiano wa Ndani, Charles Nyangi, amesema hayo kwenye maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma.
Amesema gesi hiyo pia ni muhimu kwa matumizi ya majumbani na viwandani, na hivi sasa inapatikana Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.
Amesema Serikali inaendelea kuwekeza ili kusambaza huduma hiyo katika mikoa mingine.
Pia amesema  gesi asilia hiyo  imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, hasa kwenye sekta ya uzalishaji wa umeme, na kutolea mfano uwekezaji wa Serikali katika miradi ya umeme wa bwawa ambayo inachangia kuongeza upatikanaji wa nishati endelevu.
Amesema kupitia usimamizi wa PURA, Serikali inalenga kuhakikisha kwamba rasilimali za mafuta na gesi asilia zinawanufaisha Watanzania kwa kuimarisha ushirikishwaji wa wazawa, kukuza ujuzi wa kitaifa na kuongeza fursa za kiuchumi.
Amesema PURA imetumia maonesho yanayoendelea jijini Dodoma kuwaelimisha wananchi kuhusu majukumu yake pamoja na fursa  zinazopatikana katika sekta ya mafuta na gesi asilia, hasa mkondo wa juu wa petroli.
“Moja ya majukumu yetu muhimu ni kuhamasisha ushiriki wa wazawa kwenye shughuli za mkondo wa juu wa petroli. Ushiriki huu umegawanywa katika maeneo matatu makuu: kupitia ajira, kupitia ujasiriamali kwa maana ya utoaji wa bidhaa na huduma, na kupitia uwekezaji,” ameeleza Nyangi.
Ameongeza kuwa kushiriki kwa PURA katika maonesho hayo kunalenga kuwaelimisha wananchi juu ya majukumu ya mamlaka na namna wanavyoweza kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo muhimu ya kiuchumi.

You Might Also Like

Bodi ya mkonge kutoa ajira kwa watu 10,000 ifukapo 2030

Kanisa La GCC Kufanya Maombi Kuelekea Uchaguzi Mkuu

Tunatatua Malalamiko Ya Wateja – Kaguo

Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa

Tanzania Kujifunza Teknolojia Ya Magari Ya Umeme Singapore- Biteko

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yatumia Zaidi Ya Bilioni 100 Kupeleka Umeme Simiyu
Next Article MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?