MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: PSPTB Yatangaza Matokeo ya Mitihani ya 32, ,Yawataka Waliokoa Alama Kujisajili Upya 
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > PSPTB Yatangaza Matokeo ya Mitihani ya 32, ,Yawataka Waliokoa Alama Kujisajili Upya 
Habari

PSPTB Yatangaza Matokeo ya Mitihani ya 32, ,Yawataka Waliokoa Alama Kujisajili Upya 

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi wetu, Dodoma
BODI ya Ununuzi na Ugavi kwa Umma Tanzania (PSPTB) imetangaza rasmi matokeo ya mitihani  ya 32 ya kitaaluma, na kuwahimiza watahiniwa waliokosa alama za kufaulu kujisajili upya na kurudia masomo yao kwa ajili ya mitihani itakayofanyika Mei 2026.
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB,  Godfred Mbanyi, amesema kuwa PSPTB ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 2007, ikiwa na jukumu la kuendesha mafunzo na mitihani ya kitaaluma katika fani ya Ununuzi na Ugavi katika ngazi mbalimbali.
Mbanyi amesisitiza kuwa PSPTB haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayekiuka kanuni na taratibu za mitihani, ikiwemo kufutiwa matokeo, kusimamishwa kushiriki mitihani kwa vipindi vitatu mfululizo, kutozwa faini au hata kifungo cha jela, ili kulinda maadili na uadilifu katika tasnia ya Ununuzi na Ugavi nchini.
Habari Picha 11011
Aidha Bodi hiyo imetoa  pongezi kwa watahiniwa waliofaulu na kutoa onyo kali kwa wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mitihani.
Mbanyi, amesema kuwa PSPTB ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 2007, ikiwa na jukumu la kuendesha mafunzo na mitihani ya kitaaluma katika fani ya Ununuzi na Ugavi katika ngazi mbalimbali.
Habari Picha 11012
Ameeleza kuwa uendeshaji wa mitihani hiyo ni utekelezaji wa matakwa ya sheria, mtaala pamoja na maombi ya muda mrefu kutoka kwa wadau wa fani hiyo.
Amesema  jumla ya watahiniwa 1,291 walidahiliwa kushiriki mitihani ya 32, ambapo watahiniwa 1,223 walifanya mitihani hiyo huku watahiniwa 68 wakishindwa kuhudhuria kwa sababu mbalimbali.
Amefafanua kuwa kati ya watahiniwa waliofanya mitihani, watahiniwa 595 sawa na asilimia 48.7 wamefaulu huku akisema  watahiniwa 589 sawa na asilimia 48.2 watalazimika kurudia masomo yao ambapo watahiniwa 39 sawa na asilimia 3.2 wamefeli na kuanza upya masomo yao katika ngazi husika.
Mbanyi amesema PSPTB inatoa pongezi za dhati kwa watahiniwa wote waliofaulu mitihani yao katika ngazi zote, pamoja na wale waliopata sifa za kutunukiwa Vyeti vya Professional Diploma, Graduate Professional na CPSP.
Aidha amewapongeza wahadhiri na wakufunzi kutoka vyuo na vituo mbalimbali vya mafunzo kwa mchango wao mkubwa katika kuwaandaa watahiniwa.
Mbanyi  amesema PSPTB imebaini na kuwakamata watahiniwa wawili wa ngazi ya CPSP wakijihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa taratibu za mitihani, baada ya kukutwa wakiwa na karatasi ambazo inasadikika zililenga kuwasaidia kujibu mitihani yao.
Habari Picha 11013
Alieleza kuwa Bodi ya Wakurugenzi imeielekeza Kamati ya Usajili na Nidhamu kushughulikia suala hilo, na endapo wahusika watapatikana na hatia, hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa kanuni zilizopo. Kwa sasa, matokeo ya watahiniwa hao yamezuiliwa wakisubiri kusikilizwa.
Ametoa wito kwa wazazi, wadhamini na waajiri kuwasaidia watahiniwa kwa kuwalipia ada za maandalizi na mitihani, hatua itakayosaidia kuongeza idadi ya wataalam wenye ujuzi na maarifa katika sekta ya Ununuzi na Ugavi.

You Might Also Like

Balozi Sirro: Bila Amani, Maendeleo Hayapo Kigoma

Ujenzi Jengo la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu Kuanza Kesho Dodoma

BoT Yawaalika Wachimbaji Kuwekeza Serikalini, Yatoa Elimu ya Fedha

Boti yazama abiria 14 kati ya 21 waokolewa

Rais Samia Atoa Bil. Nne Ujenzi Kiwanda Cha Kuzalisha  Nishati Mbadala  

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Hotuba ya Rais Samia Yachochea Miradi Mikubwa ya Viwanda na Bandari Bagamoyo – Mgalu
Next Article Elimu Ya Afya, Takwimu sahihi Na Ufuatiliaji Ni Muhimu Kuimarisha Huduma Za Chanjo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?