MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Profesa Nombo Azindua Miongozo Ya Usimamizi Ya Utafiti, Ubunifu COSTECH
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Profesa Nombo Azindua Miongozo Ya Usimamizi Ya Utafiti, Ubunifu COSTECH
Habari

Profesa Nombo Azindua Miongozo Ya Usimamizi Ya Utafiti, Ubunifu COSTECH

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: KATIBU Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo amezindua Miongozo ya Kitaifa ya Usimamizi wa Utafiti na Ubunifu ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Profesa Nombo amefanya uzinduzi huo Mkoani Dar es Salaam,  katika hafla iliyoandaliwa na COSTECH.
Nombo ametaja mwongozo wa kwanza  ni wa Kitaifa wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu ya Juu, Taasisi za Utafiti na Viwanda.
“Kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya ushirikiano duni kati ya vyuo vikuu, taasisi za utafiti na sekta ya viwanda.
” Hali hii imesababisha tafiti nyingi ambazo zinaendelea katika taasisi zetu za elimu ya juu kutoendana na mahitaji ya viwanda au jamii yetu.
“Mwongozo huu unakusudia kutatua changamoto hiyo kwa kuweka kanuni, taratibu na miongozo itakayorahisisha ushirikiano wa karibu kati ya taasisi hizi,” amesema.
Mwingine ni Mwongozo wa Kitaifa wa upatikanaji, uhifadhi na usambazaji wa takwimu za sayansi, teknolojia na ubunifu.
Amesema mwongozo huo unalenga kuimarisha upatikanaji, uchakataji, uhifadhi na usambazaji wa takwimu za sayansi na teknolojia kwa ufanisi zaidi.
Vile vile mwongozo wa Taifa wa uwezo wa utafiti wa kisayansi  na nne ni Mwongozo wa Kitaifa wa ubunifu.
Amesema utafiti na ubunifu ni nyenzo muhimu katika kuchagiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kwani nchi zote zilizoendelea duniani zimefanikiwa kutokana na uratibu na uwekezaji madhubuti katika masuala hayo.
Profesa Nombo amesema kupitia Mradi wa Mageuzi yaKiuchumi kupitia Elimu ya Juu (HEET), serikali imewekeza dola za kimarekani milioni 425 sawa na Sh. Trilioni 1.1 katika miundombinu ya elimu, vifaa vya kisasa vya kufundishia, kuimarisha ushirikiano baina ya vyuo vikuu na sekta ya viwanda.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu amesema tume hiyo ni miongoni mwa wanufaika 23 wa mradi wa HEET, ambao katika tume hiyo umelenga kuimarisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
Pia amesema mradi huo umelenga kukuza na kuendeleza uwezo wa utafiti na ubunifu katika taasisi za utafiti na maendeleo ya elimu ya juu.
Vile vile kujenga uhusiano wa kiutendaji kati ya sekta binafsi na taasisi za utafiti na maendeleo na elimu ya juu.
Ametaja eneo lingine ni kuboresha miundombinu ya kisasa ya tehama, vifaa vya huduma kwa ajili ya usimamizi wa utafiti na ubunifu.
Eneo lingine ni kukuza uwezo endelevu wa kugharamia utafiti na ubunifu, pamoja na kuimarisha uwezo wa tume katika kuratibu utafiti na ubunifu.

You Might Also Like

Dkt. Tumbo Aitaka Jamii Kuelimishwa Namna Bora Ya Kuhifadhi Taka

Sera mpya ya viwanda kuzinduliwa

Wanafunzi Wawili Wajiteka Ili Wapate Pesa Toka Kwa Wazazi wao

Watanzania Wametakiwa Wasiwachague Wanaotumia Rushwa

Someeni fani zisizo maarufu – mwalimu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article
Next Article Mbunge Kuchauka azindua kambi kuhamasisha Uchaguzi Serikali za  Mitaa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?