Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) Profesa Joseph Ndunguru amesema ili kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo inahitajika kuwekeza katika utafiti.
Profesa Ndunguru amesema hayo katika Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na maonesho lililoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Ndunguru amesema hayo wakati akitoa mada kuhusu matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika kuleta mageuzi kwenye sekta ya kilimo.
“Tunashukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu ameongeza bajeti ya utafiti pia kufanya kilimo kinachotumia matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
” Kwa sababu teknolojia zimebadilika sana ziende sasa zikatusaidie katika kuleta tija katika kilimo lakini mambo mengine ya kufanya ni kushirikiana na sekta binafsi katika shughuli mbalimbali,” amesema.
Katika mada aliyowasilisha pia ameeleza kuhusu matumizi ya teknolojia za kisasa za ndege nyuki ‘drone’ zinavyoweza kusaidia kudhibiti visumbufu vikiwemo nzige.
“Na hii ni kitu muhimu sana ndio moja ya kitu ambacho kinawavutia sana vijana kuingia katika kilimo, Ni matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu,” amesema.