Na Lucy Lyatuu
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa onyo kali Kwa waganga wa tiba mbadala kuacha kufanya ramlo chonganishi na kuacha tabia ya kuwapa masharti baadhi ya wateja wao namma ya kupata utajiri.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo,Jumanne Muliro amesema hayo Leo Dar es Salaam na kuongeza kuwa waganga watakaobainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Amesema tayari Jeshi hilo limefanya kikao na waganga wanaojulikana kama wa tiba mbadala 80 Kwa lengo la kuwaelimisha kuacha kujihusisha au kufanya ramli chonganishi ikiwa ni pamoja na kuacha tabia kuwapa masharti baadhi ya wateja wao.
Amesema masharti wanayowapa wateja wao kuwa ili wafanikiwe kwenye biashara na kupata utajiri kuwa lazima wafanye vitendo vya kulawiri au kuwabaka watoto wadogo.
“Katika hili Jeshi limetoa tahadhari na kuwaonya vikali na watakaobainika hatua zitachukuliwa,” amesema.
Muliro amesema Jeshi hilo linaendelea kushuhulikia matukio ya kikatili dhidinya watoto na wanawake yanayohusisha vitendo vya kulawiri na kubaka ambavyo wakati mwingine husababisha waganga kupoteza maisha.