Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa Miraji Issa (29) Mkazi wa Tandale na wenzake wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya raia wa China aliyefahamika kwa jina Liu Qianhu Jiangxi (48), Mfanyakazi wa Kampuni ya Hope Recycling Bonde la Msimbazi Ilala.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema hay oleo Oktoba saba, 2024 alipotoa taarifa ya tukio hilo kwa Vyombo vya Habari.
Amesema marehemu aliuawa katika tukio la kihalifu Septemba 28 mwaka huu, ambapo watuhumiwa hao baada ya mauaji waliiba baadhi ya vitu vya kampuni ya PTC investiment ambavyo vimepatikana baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi lao katika kutoa taarifa na kuahidi kutokuwa na huruma kwa wahalifu na kuendelea kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria.