Na Lucy Lyatuu
MAMLAKA ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) imesema serikali imetoa kibali maalum kwa ajili ya kushughulikia maombi ya mabadiliko ya taarifa kwa waliotumia nyaraka za kughushi pamoja na waliotoa taarifa za udanganyifu walipojisajili kwa Mamlaka hiyo.
Imesema kibali hicho maalum kimetolewa kwa muda maalum wa mwaka mmoja na kwamba wenye changamoto za taarifa hizo kujitokeza na kwenda kwenye ofisi za NIDA za wilaya wakiwa na viambatanisho vinavyotakiwa ili kufanya marekebisho wanayohitaji katika muda uliopangwa.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji amesema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kuongeza kuwa kibali cha maombi hayo kinahusisha makundi mbalimbali ikiwemo waathirika wav yeti vya kughushi, waliofukuzwa katika ajira za serikali kutokana na kutumia vyeti vya shule vya kugushi ambapo pia walitumia vyeti hivyo kujisajili NIDA.
Imesema kundi lingine ni watu waliotumia majina ya watu wengone kupata elimu,watu wlaiotoa taarifa za uongo au udanganyifu katika usajili wa NIDA na raia wa Tanzania waliojisajili kama wakimbizi.
Kaji amewataka wananchi wa makundi hayo kufika katika Ofisi za NIDA za wilaya wakiwa na nyaraka zinazohitajika ili kushughulikia maombi ya mabadiliko hayo.
Amesema watu hao watalazimika kuwa na viambatanisho vya lazima Pamoja na vya ziada kama watakavyoelekezwa.

Amevitaja viambatanisho hivyo kuwa ni Pamoja na nakala ya vyeti halisi vya elimu,cheti cha kuzaliwa kilichohakikiwa na RITA Deep Pool iliyosajiliwa na gazeti la serikali na nyaraka nyingine itakayotakiwa na Ofisi za NIDA.
Amesema maombi yatakayofanyiwa kazi ni yale yatakayokidhi masharti na vigezo vilivyowekwa baada ya wahusika kuwasilisha nyaraka zinazotakiwa kwa ajili ya kuthibitisha taarifa zao.
Aidha Mamlaka hiyo imesema kwa kuwa kibali hicho kimetolewa kwa muda maalum, wale wenye changamoto za taarifa zao kujitokeza na kwenda kwenye ofisi za NIDA za wilaya wakiwa na viambatanisho vinavyotakiwa ili kufanya marekebisho wanayohitaji katika muda uliopangwa.
Kadhalika inawaomba wananchi kutoa taarofa sahihi na za ukweli wanapokuwa wakijisajili NIDA kwa ajili ya utambulisho wa taifa kw akuwa kutoa taarifa zisizo sahihi au kufanya udanganyifu wa taarifa wakati wa usajili ni kosa kwa mujibu wa sheria ya usajili na utambuzi wa watu.

