Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa CCM ambaye ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Septemba mosi, 2024 ataongoza kikao cha Kamati Kuu Maalum.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashautlri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla imeeleza hilo.
Taarifa hiyo imesema kikao hicho ambacho kilikuwa kifanyike Jumatatu Septemba 2, 2924 kimebadilishwa na kufanyika kesho.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kikao hicho kimetanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu, leo Agosti 31 jijini Dar es Salaam.