MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mwelekeo Mpya wa Viwanda: Safari ya Siku 100 za Mageuzi ya Kiuchumi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Mwelekeo Mpya wa Viwanda: Safari ya Siku 100 za Mageuzi ya Kiuchumi
Makala

Mwelekeo Mpya wa Viwanda: Safari ya Siku 100 za Mageuzi ya Kiuchumi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
7 Min Read
Na Lucy Ngowi
NDANI ya siku 100 za Serikali ya Awamu ya Sita, muhula wa pili, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya viwanda imeendelea kuonesha mafanikio yanayopimika na yenye kugusa maisha ya wananchi.
Utekelezaji wa ahadi za uchaguzi umejikita katika kukuza ajira, kuimarisha uwekezaji, kurasimisha biashara, kuongeza thamani ya mazao na kupanua masoko, huku vijana wakiwa kiini cha mkakati huo.
Habari Picha 11222
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, anasema kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), jumla ya Sh. Milioni 821.7 zimetolewa kwa vijana wajasiriamali katika mikoa 19 kupitia mifuko ya Taifa ya Maendeleo ya Wajasiriamali (NEDF) na Mpango wa Dhamana ya Mikopo (CGS).
Kwamba, mikopo hiyo imezalisha ajira 546 za moja kwa moja, zikiwamo 436 za vijana, pamoja na zaidi ya ajira 1,000 zisizo za moja kwa moja katika sekta za viwanda, kilimo, ufugaji na huduma.
Waziri Kapinga anasema, mpango huo ni endelevu na utaendelea kupanuliwa ili kuongeza upatikanaji wa mitaji na kukuza viwanda katika kila wilaya.
Habari Picha 11223
Katika kuimarisha viwanda na kongani za uzalishaji, Kapinga anasema, serikali imekamilisha hatua za awali za kuanzisha mitaa na kongani za viwanda katika mikoa 11, zikilenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini.
Pia anasema, ujenzi na ukarabati wa miundombinu umeanza, huku baadhi ya maeneo yakikamilika.
Anaeleza kuwa, uzinduzi wa kongani za SIDO umeandaliwa katika mikoa ya Kigoma, Morogoro, Mbeya na Singida, zikitarajiwa kuwa na zaidi ya viwanda 120 na kutoa maelfu ya ajira za moja kwa moja, nyingi zikiwa za vijana.
Habari Picha 11224
Aidha, maeneo maalum ya viwanda vya vijana yametengwa Kigamboni (Dar es Salaam), Nyakato (Mwanza), Azimio (Arusha), Songwe (Mbeya), Uvinza (Kigoma) na Mbinga (Ruvuma).
Kwa mujibu wa Waziri Kapinga, Mpango Maalum wa Kukuza Viwanda unalenga kuongeza viwanda 9,048 na kuzalisha ajira zaidi ya milioni 6.5 ndani ya miaka sita.
“Hatua hiyo itaongeza kipato cha wakulima kupitia uongezaji thamani na kusogeza viwanda karibu na maeneo ya uzalishaji,” anasema.
Sekta Binafsi na Uwekezaji
Pia anaeleza, sekta binafsi inaendelea kuwa mhimili wa ajira nchini.
Kwani ndani ya siku 100, uwekezaji umeimarika katika maeneo mbalimbali.
Kwamba, Kongani ya Kilimanjaro Industrial Park, Kigamboni, imeanza uzalishaji wa majaribio katika kiwanda cha mabati na kwa sasa ina viwanda vitatu vinavyofanya kazi, vikitoa ajira takribani 5,000.
Habari Picha 11225
Kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC),  wawekezaji wakubwa wamevutiwa katika Kongani ya Shirika la Uhandisi na Utengenezaji wa Zana za Kilimo Tanzania (TAMCO), akiwemo Hyundai Automobile Manufacturing kwa ajili ya kuunganisha magari, pamoja na wawekezaji wa magari ya umeme na wazalishaji wa chakula cha mifugo.
Miradi ambayo, inatarajiwa kuzalisha zaidi ya ajira 1,000 za moja kwa moja.
Maelezo yake ni kwamba, Kiwanda cha viuadudu cha Kibaha (TBPL) kimezalisha maelfu ya lita za dawa kwa soko la ndani na nje, kupunguza uagizaji na kuchangia udhibiti wa magonjwa.
Habari Picha 11226
Vilevile, kongani za Kwala, Kamaka (Hifadhi ya Kisasa ya Viwanda), Goodwill (Mkuranga) na Benjamin Mkapa (Mabibo) zimeendelea kuvutia uwekezaji na kutoa maelfu ya ajira.
Uongezaji Thamani na Teknolojia
Anasena, kupitia TEMDO, viwanda vitatu vya kuongeza thamani vimekamilika na kuanza uzalishaji ikiwemo,  kiwanda cha nishati jadidifu Nyang’wale (Geita), mtambo wa kukamua alizeti Arusha, na kiwanda cha kuchakata muhogo Handeni (Tanga).
“Kwa pamoja, vinatarajiwa kutoa zaidi ya ajira 300 za moja kwa moja na 700 zisizo za moja kwa moja,” anasema.
Habari Picha 11227
Aidha, kiwanda cha kusafisha mafuta ya kula kinachofungwa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kitaongeza ubora wa mafuta ya alizeti, mawese na parachichi, na kutoa ajira kwa vijana.
Urasimishaji wa Biashara na Ubunifu
Waziri Kapinga anasema, kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ndani ya siku 100 zimesajiliwa kampuni 4,233, zikiwamo 2,915 za vijana, majina ya biashara 7,498 (4,742 ya vijana); alama za biashara 881, leseni za viwanda 141, na leseni za biashara Kundi “A” 4,907.
“Hatua hii imeongeza fursa za mikopo, zabuni na ushiriki katika masoko rasmi,” anasema waziri huyo.
Mapendekezo ya marekebisho ya sheria nne za biashara yamewasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kupunguza urasimu na kuboresha mazingira ya uwekezaji.
Habari Picha 11228
Anaongeza kuwa, kupitia Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), vijana 1,240 wamepata mafunzo ya ujasiriamali, 228 wamesajiliwa katika vituo vya atamizi za biashara, na klabu tisa za ujasiriamali zimeanzishwa mashuleni.
Programu ya atamizi za biashara imeanza, ikiwajumuisha vijana 278 katika miradi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na uzalishaji.
Ubora na Masoko
Kuhusu ubora wa masoko, Waziri Kapinga anasema,  Kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), programu ya Samia Ubora Kliniki imetoa mafunzo bure kwa wajasiriamali 1,059 na kupima sampuli 800 za bidhaa bila gharama.
Kwamba, bidhaa 192 zimetunukiwa alama ya ubora, hatua inayorahisisha upatikanaji wa masoko ya ndani na nje.
Anasema ujenzi wa ofisi za kanda Arusha, Dodoma na Mwanza unaendelea kuimarisha huduma.
Kwa upande wa masoko, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imewezesha watumiaji 26,314 kutumia Tovuti ya Biashara ya Tanzania kupata taarifa za biashara.
Pia Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Biashara na Uwekezaji pamoja na Programu ya TanTrade umefikisha taarifa za masoko kwa wafanyabiashara 5,116.
Vile vile, Nembo ya
‘ Made in Tanzania’  imesajili huduma na bidhaa 30, huku kampuni 698 zikiratibiwa kushiriki masoko ya kimataifa.
Habari Picha 11229
Kwa ujumla, mafanikio ya siku 100 yanaonesha mwelekeo thabiti wa kujenga uchumi wa viwanda unaowajumuisha vijana, kuimarisha sekta binafsi na kupanua masoko ya ndani na nje ya nchi.
Serikali imeweka msingi imara wa kuongeza thamani ya rasilimali za ndani, kukuza ajira zenye staha na kuimarisha ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la kimataifa.
Kupitia amani, utulivu na ushirikiano kati ya Serikali na wananchi, sekta ya viwanda inaendelea kuwa injini muhimu ya ajira, kipato na maendeleo endelevu ya Taifa, ikiimarisha safari ya kuelekea uchumi shindani na jumuishi kwa kizazi cha sasa na kijacho.

You Might Also Like

Profesa Ndunguru: Mtafiti Aliyejitoa Kusaidia Dunia Kupata Chakula Cha Baadae

Polisi Dar yashikilia watatu kwa mauaji ya mfanyakazi wa Kampuni ya Hope Recycling

UDSM Chang’ara STICE – 2024 Kupitia Mhadhiri Na Mtafiti Wake Dkt. Mmochi

Wanachuoni Katika Mawasilianao ya Utamaduni kati ya China na Afrika

Waziri Kombo: Ushirikiano Wa China, Tanzania Umeleta Maendeleo Ya Kijani

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Watu Wenye Ulemavu Nchini Wafikia Mil 5.3
Next Article JAB Yasisitiza Ithibati Kama Njia ya Kuimarisha Ubora na Uaminifu wa Habari
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Makamu wa Rais Asisitiza Ubunifu, Uwekezaji Soko La Hisa La Dar es Salaam
Habari February 13, 2026
JAB Yasisitiza Ithibati Kama Njia ya Kuimarisha Ubora na Uaminifu wa Habari
Habari February 13, 2026
Watu Wenye Ulemavu Nchini Wafikia Mil 5.3
Habari February 12, 2026
MAIPAC Yasisitiza Maadili Na Usalama Kwa Waandishi Wa Habari
Habari February 12, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?