Na Mwandishi Wetu
LINDI: MGOMBEA urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim, amesema inashangaza kuona mikoa ya Lindi na Mtwara yenye rasilimali za makaa ya mawe, gesi na korosho bado ina umaskini mkubwa.
Akizungumza na wananchi wa Lindi Mjini, Mwalim amesema umasikini huo unasababishwa na wananchi kuendelea kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mtetezi wao. Aliwataka wananchi kuiamini na kuichagua CHAUMMA ili iwe mkombozi wao.

“Simameni na mgombea wa CHAUMMA ili tunyooshe nchi… hakuna litakaloshindikana,” amesema.
Aidha, amesisitiza kuwa CHAUMMA haitakubaliana na mfumo wa stakabadhi ghalani, akieleza kuwa mkulima anatakiwa kuvuna korosho yake na kuuza popote anapotaka ilimradi alipe ushuru wa serikali.
“Vijana wenzangu, nakwenda kupambana na ajira kwa vijana… sitaliangusha Taifa hili,” amesema.