Mwandishi Wetu
ARUSHA: MTOTO mwenye umri wa miaka sita ni miongoni mwa washindi tisa wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quraan Tukufu yaliyoandaliwa na Jukwaa la vijana wa Kiislam Mkoa wa Arusha.
Katika Mashindano hayo yaliyoshirikisha vijana 31 katika kuhifadhi na kusoma vyema juzuu tatu,tano na 10 , Mgeni Rasmi alikuwa ni Sheikh wa mkoa Arusha, Shaban Juma.

Mtoto huyo wa miaka sita, Is’haqa Yahya Giriba amezawadiwa zawadi mbalimbali ikiwepo luninga ya nchi 24, nafasi ya pili alishinda Mohamed Abdalah ambaye alizawadiwa radio kubwa huku nafasi ya tatu akishinda Nasmah Omar ambaye pia alizadiwa radio na zawadi nyingine.
Katika mashindano hayo ambayo yalifanyika ukumbi ya Arusha Mall na kuhudhuriwa na mamia ya watu, Sumaiya Abubakar ameshinda katika kusoma na kuhifadhi juzuu tano na kuzawadiwa TV nchi 24.

Mshindi wa pili wa juzuu tano alikuwa Sophia Rajab aliyezawadiwa TV wakati mshindi wa tatu Tamir Idrisa alizawaduwa zawadi kadhaa ma Radio kubwa.
Katika mashindano hayo ambayo mdhamini mkuu alikuwa ni Benki ya Amana,Ibrahim Ayoub alishinda juzuu 10 na kuzawadiwa zawadi kem kem ikiwepo TV nchi 32.
Mshindi wa pili alikuwa ni Yusra Yasin ambaye alizawadiwa zawadi mbalimbali na TV nchi 24 huku Nuswiba Nashir alishinda nafasi ya tatu na kuzawadiwa TV na zawadi nyingine.

Sheikh wa mkoa Sheikh Shaban Juma akizungumza katika mashindano hayo, alipongeza jukwaa la vijana kuandaa mashindano hayo ambayo ni muhimu sana katika kuhamasisha usomaji wa Quraani tukufu.
Sheikh Shaban Juma amesema Mwenyezimungu amehimiza usomaji wa quraani tukufu kwani jambo zuri na linafaa kuendelezwa.
Amewataka waislam na vijana wa kislam mkoa Arusha,kuendeleza usomaji mzuri wa Quraani kwani kuna manufaa makubwa na thawabu nyingi hasa kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhan.
Sheikh wa mkoa pia amewataka Waislam mkoa Arusha,kuunga mkono kazi nzuri ambazo zinaendelea kufanywa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Meja wa jiji la Arusha,Maximillian Irange akizungumza katika mashindano hayo ,amewataka Waislam mkoa Arusha kuendeleza umoja na.mshikamano baina yao
Meneja wa Amana Benki mkoa Arusha, Ally Mdee amesema lengo la benki hiyo kudhamini mashindano hayo ni kuwaunganisha waumini katika mambo ya kheri.
Amesema Amana benki ina huduma mbalimbali ikiwepo kuweka fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kwenda kuhiji Makka na kwenda Umra.

“Pia tunatoa mikopo kwa misingi ya Sharia hivyo karibuni”amesema
Amir wa Jukwaa la Waislam mkoa Arusha,Kassim Digega aliwashukuru mamia ya waislam kwa kuhudhuria mashindano hayo na Benki ya Amana kuwa mdhamini mkuu.
Degega amesema mashindano hayo ya kwanza kuandaliwa na jukwaa la vijana wa Kiislam mkoa Arusha yamekwenda vizuri na Allah akipenda mwakani yatakuwa makubwa zaidi .
Katika mashindano hayo jukwaa la vijana lilitoa tende kwa watu wote ambao walishiriki na pia zawadi mbalimbali ikiwepo misahafu na Juzuu.