MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mtasingwa Aitaka Serikali Kuwatengea Eneo Wafanyabiashara wa Senene Bukoba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mtasingwa Aitaka Serikali Kuwatengea Eneo Wafanyabiashara wa Senene Bukoba
Habari

Mtasingwa Aitaka Serikali Kuwatengea Eneo Wafanyabiashara wa Senene Bukoba

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
Dodoma: MBUNGE wa Bukoba Mjini, Johnston Mtasingwa, amesema zaidi ya wafanyabiashara wa senene 1,000 katika jimbo lake hawana eneo rasmi la kufanyia shughuli zao, hali inayowalazimu kufanya biashara pembeni mwa eneo ambalo kwa sasa linajengwa jengo la kituo cha mabasi.
Akizungumza bungeni leo Januari 30, 2026, Mtasingwa aliitaka serikali kutenga fedha za ziada ili kupanua jengo hilo na kuweka eneo maalum kwa ajili ya wafanyabiashara hao wa senene.
Pia aliomba Waziri husika kutembelea jimbo la Bukoba Mjini ili kujionea hali halisi na kupata fursa ya kuzungumza na wafanyabiashara hao.
“Je, serikali haiwezi kuongeza fedha kidogo kwenye mradi huo ili hawa wafanyabiashara wapate sehemu sahihi ya kufanyia shughuli zao? Na ni lini Mheshimiwa Waziri ataambatana na mimi kwenda kuona maeneo hayo na kuzungumza na wafanyabiashara wa Bukoba Mjini?” alihoji Mtasingwa.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Denis Londo, alisema serikali kwa kushirikiana na Manispaa ya Bukoba imeanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa soko la senene katika eneo la Soko la Mjini, maarufu kama Senene Complex.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwakusanya wafanyabiashara wote wa senene katika eneo moja na kuwawezesha kufanya biashara katika mazingira rafiki na salama.
Aliongeza kuwa suala la uwezeshwaji wa wafanyabiashara linaendelea kuratibiwa kupitia serikali za mitaa, na kwa kuwa nchi inaelekea katika mchakato wa bajeti, ni matarajio ya serikali kwamba ombi hilo litaingizwa rasmi katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.
“Wizara ya Viwanda na Biashara itaendelea kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge kuhakikisha serikali inaweka msukumo wa kutosha katika utekelezaji wa mradi huu,” alisema Londo, huku akithibitisha kuwa baada ya shughuli za Bunge, ataambatana na Mbunge Mtasingwa kutembelea jimbo la Bukoba Mjini.

You Might Also Like

Udiwani Kata Ya Mbabala Kizungumkuti

REA Kusambaza Majiko Banifu 10,650 Mkoa Wa Pwani

Serikali Yajizatiti Kukabiliana na Maafa – Majaliwa

Kutoka 1975 hadi 2025: TUCTA Yatimiza Ndoto Ujenzi Jengo La Biashara Arusha

COSOTA Yapokea Migogoro 136 Ndani Ya Miaka Minne

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mvua, Upepo Yaharibu Shule Lindi, Serikali Yatoa Milioni 96
Next Article Mbunge Ndoinyo Asema Imani ya Wananchi kwa Rais Samia Yazidi Kuimarika
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?