Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imepongezwa kwa kuzunguka na kutoa elimu ya ujasiriamali katika Kata zote 36 zilizopo Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kutoa uelewa wa mikopo ya halmashauri ya asilimia 10 kwa wajasiriamali wake.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ametoa pongezi hizo wakati akifungua Kongamano la Wajasiriamali lililoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
“Nampongeza Mkurugenzi wa Jiji Elihuruma na timu yake kuweza kuzunguka kwenye kata zote 36,”amesema.
Alisema halmashauri hiyo ndiyo inayotoa mikopo mikubwa kuliko zote, pia ina watu wengi kuliko halmashauri zote.
Alisema kazi inayofanywa Ilala ni kubwa inatoa mikopo kwa wanaofanya biashara katika wilaya hiyo.
Mpogolo alisema mjasiriamali hawezi kupewa fedha bila kumjulisha namna ya kutumia mikopo, hivyo mafunzo yatakayotolewa yatawawezesha kujua sheria na kanuni za mikopo.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuirejesha tena mikopo hiyo ya asilimia 10 baada ya kuisitisha Aprili mwaka jana.
Amesema Rais Samia ameona kuwe na utaratibu mpya kwa halmashauri ya jiji ambayo imeteuliwa miongoni mwa halmashauri 10 za mfano nchini mkopo utolewe kwa utaratibu wa kibenki.
Mpogolo Ài