MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mkunda: Wanawake Wapewe Nafasi Katika Uongozi wa Vyama vya Wafanyakazi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mkunda: Wanawake Wapewe Nafasi Katika Uongozi wa Vyama vya Wafanyakazi
Habari

Mkunda: Wanawake Wapewe Nafasi Katika Uongozi wa Vyama vya Wafanyakazi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DODOMA: KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Henry Mkunda, amesema shirikisho hilo litaendelea kuhimiza vyama vya wafanyakazi nchini kuweka kipaumbele kwa wanawake kwa kuhakikisha katiba za vyama hivyo zinatenga nafasi za uongozi.

Mkunda, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), ametoa kauli hiyo leo Machi 7, 2025 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na shirikisho hilo, yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Amesema shirikisho hilo linaendelea kusisitiza ushiriki wa wanawake katika vyama vya wafanyakazi kuanzia ngazi ya juu hadi matawi, ili kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maamuzi na uongozi.

Habari Picha 11340

Mkunda ametaja pia vyama vipya vinavyoendelea kujiunga na shirikisho hilo,, ikiwemo Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), kuwa vitazingatia usawa wa kijinsia katika katiba na mifumo yake ya uongozi.

“Katika vyama vya wafanyakazi tuna kamati kuanzia ngazi ya juu hadi kwenye matawi, na tunahakikisha wanawake wanapata nafasi ya kushiriki na kuongoza,” amesema Mkunda.

Habari Picha 11341

Aidha, ameiomba Serikali kuendelea kuboresha sera na mazingira ya kazi yanayowahusu wanawake, hususan wale wanaosafiri kwenda kufanya kazi nje ya nchi.

Amesema shirikisho hilo limeanza kutekeleza programu mbalimbali za kuwawezesha wafanyakazi wanaokwenda kufanya kazi nje ya Tanzania, kupitia ushirikiano wa mashirikisho ya wafanyakazi katika nchi za Kiarabu, ili kuhakikisha wanapata ulinzi na msaada wa vyama vya wafanyakazi wanapofika huko.

Mkunda amesisitiza kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii, akieleza kuwa mbali na kuwa viongozi ndani ya familia na wahusika wakuu wa malezi, pia wanachangia katika shughuli za kiuchumi na za kiimani.

Habari Picha 11341

Ameongeza kuwa kuwezeshwa kwa wanawake katika sekta ya ajira na uongozi wa vyama vya wafanyakazi ni hatua muhimu katika kuimarisha usawa na maendeleo ya kijamii nchini.

Habari Picha 11343
Habari Picha 11344

You Might Also Like

Serikali imejipanga Mkakati wa Taifa wa Matumìzi ya nishati safi ya kupikia – Mramba

Serikali Yaweka Mkazo Kukuza Tasnia Ya Ufugaji Wa Kuku

Chalamila afanya ukaguzi mwenendo wa utoaji huduma Kivuko cha Feri

Mara Yapaa: Miaka Minne Ya Mafanikio Chini Ya Rais Samia

Serikali Kupeleka Umeme Maeneo Ya Kimkakati

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mifugo Mingi Chanzo Cha Uchafuzi Maji Ziwa Victoria
Next Article Balozi Seokolo Atoa Wito Kuimarisha Biashara na Viwanda Kanda ya SADC
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wataalamu wa Fedha SADC Wakutana Pretoria Kujadili Bajeti
Habari March 9, 2026
TASFAM Yawawezesha Wanawake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kuadhimisha Siku ya Mwanamke
Habari March 9, 2026
Nyamhokya Atoa Wito kwa Wanawake Kusimama Imara Kiuchumi
Habari March 7, 2026
Balozi Seokolo Atoa Wito Kuimarisha Biashara na Viwanda Kanda ya SADC
Habari March 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?