Na Lucy Ngowi
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema nchi zinasonga mbele kwa kuwekeza kwenye sayansi, teknolojia na ubunifu
Amezungumza hayo mkoani Dar es Salaam, kwenye Mkutano wa Mawaziri na Waandishi wa Habari ulioandaliwa na Idara ya Habari – Maelezo
Amesema elimu ambayo haiandai wana sayansi wa nchi haiwezi kusonga mbele.kwani haiwezekani kuwa na madaktari wazuri bila kuwa na wana sayansi
Amesema katika mageuzi ya elimu nchini, msukumo mkubwa umewekwa kwenye mkondo wa sayansi
Pia amesema ili vijana wapende sayansi, waliweka vivutio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzisha ‘Samia Scholaship’.
“Rais Samia Suluhu Hassan alisema, vijana wanaofanya vizuri katika sayansi kidato cha sita, wasomeshwe,” amesema.
Alisema Samia scholarship inavutia vijana wenye uwezo wasome sayansi kwa kuwa bila hivyo taifa haliwezi kuendelea.
Kwa upande mwingine amesema elimu nyingine ni ya akili unde, mambo ya data sayansi, kwa kuwa dunia inaenda kasi hata masuala ya usalama wa nchi, uchumi. kilimo, benki vinategemea masuala ya akili unde
“Tanzania tuna vyuo vyetu tunafundisha lakini tumeamua kuwapeleka nchi zilizoendelea zaidi yetu,” amesema.
Kwa mujibu wa Profesa Mkenda serikali imepeleka vijana 50 Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kilichopo Arusha, kama kambi ya mafunzo ya kuwaandaa ili waje kwenda kujifunza zaidi nje ya nchi.
Alisema vijana hao, watapelekwa nje kwa utaratibu wa serikali , awamu ya kwanza itaondoka mwisho wa Januari 2026, kwenda Chuo Kikuu Afrika Kusini, na ya pili itaondoka Septemba

