MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mjadala wa Kidiplomasia Ya Kisayansi Wafanyika Marekani
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mjadala wa Kidiplomasia Ya Kisayansi Wafanyika Marekani
Habari

Mjadala wa Kidiplomasia Ya Kisayansi Wafanyika Marekani

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu, New York, Marekani

WIZARA  ya Afya ya Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (ECSA-HC) pamoja na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), wameandaa mjadala muhimu kuhusu Diplomasia ya Kisayansi katika Mkutano Mkuu wa 80 wa Umoja wa Mataifa (UNGA 80) unofanyika jijini New York, Marekani.

Mjadala huo umewakutanisha viongozi wa Serikali kutoka Afrika, watafiti, wawakilishi wa taasisi za kikanda na washirika wa maendeleo kwa lengo la kuangazia nafasi ya sayansi katika kuimarisha mifumo ya afya, kuchochea uvumbuzi, na kuimarisha ushirikiano wa kikanda kwa maendeleo endelevu ya bara la Afrika.

Habari Picha 9621

 

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya,  Jenista Mhagama,   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Afya,  Ismail Rumatila, amesisitiza umuhimu wa kutumia matokeo ya tafiti za kisayansi kutengeneza suluhisho la changamoto halisi, ikiwemo kuwekeza kwenye uzalishaji wa bidhaa za ndani ya nchi ili kupunguza utegemezi wa nje.

 

Rumatila amezitaja taasisi kama MUHAS na ECSA-HC kuwa mifano ya mafanikio ya ubunifu wa Kiafrika ambayo bara la Africa linapaswa kujivunia na kuyaendeleza.

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa ECSA-HC, Dkt. Ntuli Kapologwe, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza uwekezaji wa uwezo wa kisayansi barani Afrika, huku  akibainisha kuwa, ingawa Afrika inabeba zaidi ya asilimia 25 ya mzigo wa magonjwa duniani, bara hilo linachangia chini ya asilimia mbili  (2) ya machapisho ya kisayansi na hupokea chini ya asilimia moja (1) ya ufadhili wa utafiti na maendeleo (R&D).

 

Dkt. Kapologwe amefafanua kuwa ECSA-HC iko mbioni kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Kikanda cha Sayansi na Ubunifu jijini Arusha, kitakacholenga kukuza tafiti na uvumbuzi kama njia ya kudhibiti changamoto za kiafya barani Afrika.

Habari Picha 9622

 

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa IGAD,  Workneh Gebeyehu, na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),  Veronica Nduva, wameunga mkono wito huo, wakisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kikanda na kujitegemea katika sekta ya afya. Kutoka upande wa kifedha, Bw. Zitto Alfayo kutoka AfriExim Bank amehimiza kuwepo kwa ufadhili endelevu wa tafiti zinazoendeshwa na Waafrika kwa ajili ya Afrika.

 

Waziri wa Mambo ya Nje,  Mahmoud Thabit Kombo, akihitimisha mjadala huo kwa niaba ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango yeye amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, na jumuiya za kisayansi ni muhimu ili kuifanya sayansi kuwa dira ya maendeleo ya Afrika.

 

You Might Also Like

TARURA yaimarisha ubora wa barabara kwa kuwa na maabara mikoani

Dar Yaidhinishiwa Bil. 68 Ukarabati, Matengenezo Ya Barabara

VETA Yatafiti Dawa Ya UTI, Fangasi

Serikali  Kuja Na Mradi  Wa Kuimarisha Upatikanaji Umeme Vitongojini- Kapinga 

August 10, 2024

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article REA Kivutio Kikubwa Uuzaji Wa Majiko Banifu Kwa Bei Ya Ruzuku
Next Article Mkuu Wa Wilaya Komba Aitaka DIB Kuongeza Ulinzi Kwa Fedha Za Wananchi Katika Vikoba, SACCOS
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda
Habari October 17, 2025
Profesa Nombo: Ushirikiano wa VETA, Sekta Binafsi Waimarisha Mafunzo ya Ufundi Stadi
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?