Na Lucy Ngowi
DODOMA: SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol (TPDC), limepanga kuanzisha vituo vya gesi asilia mikoa ya Pwani, Morogoro na Dodoma katika mwaka huu wa fedha 2024/2025.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano ma Mawasiliano wa TPDC, Marie Mselem amesema hayo alipzungumza navwaandishi wa habari katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea jijini Dodoma.
Amesema kwa kuanzisha vituo hivyo, hkutasaidia mtu kusafiri
kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia gesi asilia badala ya mafuta, pia itawqfanya watu wengi kuendelea kubadilisha mifumo ya magari yao kutoka kwenye matumizi ya mafuta kwenda kwenye gesi.
“Vituo hivyo vitasaidia mtu kusafiri kutoka Dar es salaam hadi Dodoma kwa usafiri unaotumia gesi asilia. Usafiri huu ni mzuri na salama kwasababu hautumii gharama kubwa na ni rafiki kwa mazingira,” amesema.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Sophia Mwakagenda ameipongeza serikali kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi.
Amesema serikali imeendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kujenga vituo vya kujazia gesi asilia ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo Kwa wananchi.
“Serikali inastahili pongezi kwa kuendelea kuweka Nguvu kubwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi na Sasa serikali inaendelea kujenga vituo vya kujazia gesi hiyo ili kuwahakikisha wale wote waliobadilisha mfumo kutoka katika matumizi ya mafuta kuwa huduma hiyo ipo,”amesema Msellemu