Na Danson Kaijage
DODOMA: WANANCHI wa Kata ya Chang’ombe Jijini Dodoma wamepongeza mkakati wa Jeshi la Polisi kwa kuwafikia vijana kupitia michezo inayopunguza uhalifu, huku wananchi wakishiriki vikundi vya ulinzi shirikishi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amesema hayo wkjati wakisherekea ubingwa wa ligi ya mpira wa miguu iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma chini
Umoja Polisi Jamii Cup iliyo tamatika siku za hivi karibuni .
Ameipongez timu na wananchi wa kata hiyo kwa kuonyesha kiwango bora cha soka kati ya kata zaidi 14 zilizo shiriki katika mashindano hayo.
Vilevile Katabazi amesisitiza wananchi kuendelea kuchukia uhalifu na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kuchukuliwa hatua za kicheria kabla uhalifu haujatendeka.
“Chang’ombe mmekuwa mfano katika Jiji la Dodoma mmefanya vizuri katika michezo na mmebadilika tufauti na hapo awali ilivyokuwa chang’ombe ikisifika kwa uhalifu, muendelee kuchukia uhalifu na msishiriki katika uhalifu,” amesema.
Amewataka wazazi na walezi wa kata hiyo kuwasimamia watoto katika malezi na kushirikiana na Polisi Kata wa eneo hilo pindi wanapokutana na changamoto za ulinzi na usalama pamoja na kushiriki katika shughuli za maendeleo na siyo uhalifu.
Kwa upande wake mlezi wa timu ya Chang’ombe ambaye ni Polisi Kata wa kata hiyo Samweli Gwivaha ameeleza ushirikiano ulipo kati ya wananchi katika kuzuia na kutanzua uhalifu kupitia michezo.
Hata hivyo Wananchi wa kata ya Chang’ombe wamepongeza mkakati wa Jeshi la Polisi kupitia kamanda wa mkoa huo kuwakutanisha vijana kupitia michezo na kuimarisha doria ambapo wamesema kata hiyo kwa sasa amani imeendelea kutamalaki na uhalifu kufikia ukomo.
Mashindano hayo yaliokuwa na lengo la kuwakutanisha vijana katika maeneo mbalimbali kupitia michezo na kuwapa elimu ya ulinzi pamoja kuhamasisha ushiriki wa vijana hao katika vikundi vya ulinzi shirikishi.