NA MWANDISHI WETU
MBUNGE wa Liwale mkoani Lindi, Zubeir Kuchauka amezindua kambi ya vijana kwa ajili ya kuhamasisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Katika uzinduzi huo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandishika katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura .
Amewataka Novemba 27 mwaka huu wajitokeze kwenda kupiga kura ili kutimiza haki ya kimsingi ya katiba ya nchi kuchagua viongozi wanaofaa.
Amewasisitiza vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali hususani katika miradi ya maendeleo.

Amewaasa kutoshiriki katika makundi ya ovyo ili Kambi hiiyo iwe yenye matokeo chanya kwa Chama Cha Mapinduzi.
“Vijana kuwa na uadilifu na uaminifu ndio nguzo ya maisha kwa sasa na si kujiunga na makundi yasiyo na mafanikio,”amesema