RWANDA: WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, pamoja Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa wakiwa katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Akili Mnemba Barani Afrika unaofanyika Kigali, Nchini Rwanda.
Mkutano huo wa Sayansi na Teknolojia mahususi kwa ajili ya kujadili masuala ya Akili Mnemba unaohudhuriwa na Wakuu wa Nchi za Afrika, viongozi, pamoja na wadau wa Teknolojia kutoka maeneo mbalimbali ya nje na ndani ya Bara la Afrika.