KATIKA kipindi cha mwaka mzima kuanzia Januari 2024, hadi sasa, serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha maeneo mbalimbali ili kuleta tija kwa taifa.
Haya ni baadhi ya mafanikio hayo yaliyofanywa na serikali kwa kipindi chote hicho;
JANUARI MOSI, 2024: Rais Samia Suluhu Hassan alitoa agizo kuwa ikifikia Julai, SGR iwe imeanza.
Samia alitoa agizo hili alipokuwa akiainisha mipango ya serikali kwa mwaka 2024.
JANUARI 10, 2024: SAMIA: Tutatawala soko la karafuu ulimwenguni.
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema serikali kupitia balozi zake na majukwaa mbalimbali yataendelea na jitihada za kufungua masoko ya zao la karafuu ili kuongeza uuzaji wa zao hilo nje ya nchi.
Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na wananchi katika tukio la azinduzi wa jengo la Kitega Uchumi la Zanzibar State Trade Cooperation – Pemba visiwani Zanzibar.
JANUARI 23, 2024: Nchi ipo salama
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda, amethibitisha kuwa amani na usalama wa nchi upo vizuri.
JANUARI 25,2024 Rais samia asifiwa kuimarisha demokrasia
Falsafa yake ya 4R kwa vitendo yagusa wengi, Mbowe ampongeza.
MACHI 12, 2024 Bajeti serikali juu kwa asilimia 11.2
Yafikia sh. Trilioni 49.3, ya sasa mafanikio kibao, sababu uchumi kuimarika zatajwa.
APRILI 27, 2024 Sherehe miaka 60 ya Muungano yafunika
Gwaride, makomandoo, tarabushi vyakonga nyoyo
Viongozi Afrika, Kimataifa Waipa ‘tabo’ Tanzania
Samia aagiza 4R zitekelezwe, uwajibikaji
wafungwa 1,082 wasamehewa
APRILI 30, 2024 Serikali kulipa madeni ya vyombo vya habari
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema atamwambia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Viongozi Wakuu wa serikali wazisihi wizara na Taasisi za Umma kuanza kulipia madeni ya matangazo wanayodaiwa na vyombo vya habari.
Biteko amesema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma wa 13 wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF), Jijini Dodoma.
MEI 12, 2024 Majaketi yenye camera kudhibiti rushwa trafiki
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuharakisha mchakato wa matumizi ya majaketi yenye kamera kwa askari wa usalama barabarani, ili kukomesha vitendo vya rushwa ambavyo kwa sehemu, vimekuwa sababu ya ajali.
Dkt. Mpango ameyasema hayo jijini Dodoma, alipokuwa akifungua kituo kipya cha polisi cha daraja ‘A’ cha wilaya ya kipolisi Mtumba pamoja na ugawaji wa magari 21.
JUNI 14, 2024 Safari ya kwanza SGR
Safari ya kwanza ya treni ya umeme (SGR), kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam imeanza rasmi Juni 14, 2024.
Treni hiyo ilianza Safari kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro saa 12 asubuhi na ilifika mkoani humo saa 1:59 asubuhi
JULAI 11, 2024 Mikopo asilimia 10 yaiva
RAIS Samia Suluhu Hassan ametangaza kurejesha tena utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kuanzia July, 2024 kwa utaratibu wa kutumia Benki kwa Halmashauri 10 za majaribio.
Halmashauri hizo ni Majiji ya Dar es Salaam na Dodoma, Manispaa za Kigoma Ujiji na Songea, Miji ya Newala na Mbulu, Wilaya za Siha, Nkasi, Itilima na Bumbuli.
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ametoa taarifa hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo April 16,2024 wakati akitoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024/2025.
JULAI 16, 2024 Udart kuingiza mabasi 100 mwendokasi
MSAJILI wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema Serikali ipo mbioni kuongeza mabasi 100 kwenye Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka
Mabasi hayo mapya yataenda kujikita katika njia kuu tu.
Sambamba na hilo Serikali yenye umiliki wa asilimia 85 kwenye mradi huo inakwenda kuongeza kampuni nyingine itakayosaidiana na Kampuni ya Usafirishaji ya Mabasi yaendayo Haraka(UDART)katika utoaji huduma
SEPTEMBA 2, 2024 Miaka 60 ya JWTZ – Tuko Imara
Rais Samia Suluhu Hassan, ataja msingi wa uimara wa jeshi na maboresho yaliyofanyika, akitaka matumizi zaidi ya teknolojia.
DISEMBA 24, 2024 Biashara saa 24 Dar mwezi ujao
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametangaza kuwa Januari, 2025 utafanyika uzinduzi mkubwa Kariakoo wa biashara Kufanyika masaa 24.
Chalamila ameyasema hayo leo Desemba 23, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.
Imeandaliwa na Mwandishi Lucy Ngowi: