MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mara Yapaa: Miaka Minne Ya Mafanikio Chini Ya Rais Samia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mara Yapaa: Miaka Minne Ya Mafanikio Chini Ya Rais Samia
Habari

Mara Yapaa: Miaka Minne Ya Mafanikio Chini Ya Rais Samia

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danso Kaijage
UONGOZI wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne,  katika Mkoa wa Mara umeonesha mageuzi makubwa kwenye nyanja mbalimbali hususan usalama, afya na elimu, mambo yanayogusa moja kwa moja ustawi wa jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evance Mtambi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO,.
Amesema hatua zilizopigwa katika kipindi hicho zimeimarisha maisha ya wananchi na kupunguza changamoto ambazo kwa muda mrefu ziliwakabili wakazi wa mkoa huo.
Amesema  usalama katika mkoa huo, hasa kwenye maeneo ya mipakani, umeimarika kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma kutokana na ushirikiano baina ya vyombo vya dola, pamoja na elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa amani zimesaidia kudhibiti matukio ya uhalifu na biashara haramu mpakani.
“Katika miaka ya nyuma kulikuwa na changamoto za usalama katika mipaka yetu, lakini kupitia juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, hali sasa ni tulivu. Wananchi wanafanya shughuli zao bila hofu, na hiyo inachangia uchumi wa eneo letu kukua,” amesema.
Katika sekta ya afya, Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa hospitali kubwa na ya kisasa imejengwa, ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Mara na hata wageni kutoka mataifa jirani.
 “Hospitali hii si tu inahudumia wananchi wa Mara, bali pia imeandaliwa kwa viwango vya kimataifa kiasi cha kupokea wagonjwa kutoka nje ya nchi. Hili ni jambo la kujivunia,” amesema.
Kwa upande wa elimu, Mtambi ameeleza shule mpya zimejengwa na ukarabati mkubwa wa miundombinu ya zamani kufanyika.
Ametaja pia ongezeko la walimu na vifaa vya kujifunzia kuwa miongoni mwa mafanikio muhimu yaliyofanikishwa kwa juhudi za serikali.
Aidha, amesisitiza kuwa sekta ya kilimo na ufugaji imekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi katika mkoa huo, Kupitia uwekezaji katika pembejeo bora, elimu ya kisasa kwa wakulima na wafugaji pamoja na masoko ya uhakika.
 “Wananchi sasa wanaona kilimo na ufugaji kama biashara, si kazi ya kujikimu tu. Hii ni hatua muhimu kwa mkoa wetu na kwa taifa kwa ujumla,” amesema.

You Might Also Like

TUCTA Yaainisha Mambo Matano Yanayohitaji Hatua Za Haraka

Mongella Atoa Maagizo Maalum Kwa Viongozi CCM

Sierra Leone Yaipongeza TARURAUjenzi Wa Madaraja, Barabara Za Mawe

Fanyeni kazi kwa bidii kulinda taswira ya TARURA

Dkt. Bwana: Tunafanya utafiti wa mbegu kutatua changamoto za wakulima

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yazindua Mafunzo Ya Mtandao Ya Afya Moja
Next Article Tanzania Yaingia Saba Bora Duniani  Kwa Uzalishaji Wa Pamba Hai
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim
Habari September 14, 2025
Heshima ya Udaktari Ni Mwito wa Kulitumikia Taifa: Dkt Ikomba
Habari September 14, 2025
Rais Wa CWT Suleiman Ikomba Sasa Ni Daktari
Habari September 13, 2025
Salum Mwalim: Nitarejesha Hadhi ya Kanda ya Ziwa na Kuinua Zao la Pamba
Habari September 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?