Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 06, 2024 amewasili Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kufungua Semina elekezi kwa viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Semina hiyo ya siku mbili imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali.