Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 17, 2024 amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA, linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya Maonesho kwenye Kongamano hilo, Majaliwa ameipongeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanasimamia ukuaji wa Sekta ya TEHAMA.
Pia Majaliwa amewataka vijana kutumia fursa ya Uwekezaji unaofanya na Serikali katika sekta ya TEHAMA ili kukuza uchumi binafsi na Taifa kwa ujumla
Kaulimbinu ya Kongamano hilo ni “Kutumia Uwezo wa Akili Mnemba na Robotiki kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii”.