Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), inawakumbusha madereva na wamiliki wa Mabasi Maalum ya Kukodi, kuzingatia matumizi sahihi ya kitufe cha utambuzi wa dereva.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Salum Pazzy ameeleza hayo katika taarifa ya umma juu ya matumizi ya kitufe hicho.
“Madereva wasio na kitufe hicho wafike Ofisi za LATRA zilizo karibu ili kusajiliwa na kuunganishwa kabla ya Januari12, mwaka huu ili kurahisisha kazi hii,” amesema Pazzy.
Amesema mamlaka hiyo itafanya wa vitufe hivyo kwenye baadhi ya maeneo ya barabara ambayo mabasi husimama.
Awali amesema kwa mujibu wa kanuni za LATRA za magari hayo ya kukodi za mwaka 2020, yanapaswa kuunganishwa na Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari.