Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema hapa nchini Kiswahili kimeanza kufubazwa, kwa kuyapa maana isiyo sahihi maelezo ya kawaida ya lugha hiyo.
Kabudi amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini, leo Februari 13, 2025.
Amesema, ” Kumeanza kuwa na changamoto ya kudumaza Kiswahili, maana ya kuwa legalese, kwa kutumia utajiri wa lugha ya kiswahili na kurudia maneno yale yale kwa kika jambo.

” Tatizo sasa limeanza kuwa sugu ni kubananga lugha ya kiswahi. Tumeanza kusena uyu siyo huyu. Uyo sio huyo, Ana sio Hana,” amesema.
Kabudi amesema kwa hiyo kiswahili kinabanangwa, matokeo yake watumiaji wa lugha ya kiswahili katika nchi zinazozubguka Tanzania, watanzania ni wazungumzaji wa kiswahili lakini siyo mahiri tena kwa kiswahili fasaha na sanifu.
Kwa upande Wake Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari amesema mamlaka hiyo imejiwekea utaratibu wa kukutana na vyombo vyote vya habari, mara moja kwa mwaka.

Amesema lengo la kukutana ni kushauriana, kuelomishana pamoja na kutafuta majibu ya changamoto.
“Leo ni siku ya redio duniani. Kaulimbiu ni ‘Redio na Mabadiliko ya tabia nchi’,” amesema.

Anaeleza kuwa vyombo vya habari vinapaswa kutoa taarifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ili kuiwezesha jamii kuchukua tahadhari zote zinazoendelea na mabadiliko hayo.