Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Waandishi wa Habari Dar es salaam (DCPC), kimemchagua Bakari Kimwanga kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kura 68.
Kati ya kura hizo nane za hapana, na zilizoharibika ni tano.
Baada ya kuchaguliwa, Kimwaga amesema ataibadilisha klabu hiyo ikiwemo eneo la nidhamu kwa kuwa ndio msingi wa maendeleo.
Awali matokeo hayo yalitangazwa na Mwenyekiti wa Kamati huru ya uchaguzi, Wakili wa Kujitegemea, Raphael Awino.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti, Mary Geoffrey, amepata kura 70 za ndiyo, saba za hapana huku nne zikiwa zimeharibika.
Wajumbe waliochaguliwa ni Selemani Jongo kura 69, Penina Malundo (62), Andrew Msechu (67) Khamis Miraji (59) na Veronika Mrema (69).
Awino pamoja na Katibu wa Tume Huru ya Uchaguzi, Janeth Jovin, wamepongeza wanachama wa DCPC kwa kufanya uchaguzi kwa amani.