MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kikwete: Waambieni Tunataka Maendeleo Sio Maneno
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kikwete: Waambieni Tunataka Maendeleo Sio Maneno
Habari

Kikwete: Waambieni Tunataka Maendeleo Sio Maneno

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

GEITA: RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa CCM kuweka mbele maslahi ya chama, pamoja na kudumisha umoja na mshikamano.
Kikwete amezungumza hayo alipohutubia katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika katika Kata ya Igulwa, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.
“Wekeni mbele maslahi ya Chama chetu, watajitokeza watu mbalimbali kuja kugombea nafasi mbalimbali wapokeeni lakini wakitokea wenye maneno tu waambieni sie tunataka maendeleo sio maneno,” amesema Kikwete.
Pia ameupongeza uongozi wa CCM Wilaya ya Bukombe kwa Mkutano Mkuu Maalum wa kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimbo la Bukombe kwa mwaka 2020-2025.
“ Nawapongeza kwa kuandaa Mkutano huu kwa kuwa unakidhi takwa la katiba ya CCM kwa kuwa inawezesha kupima mlipotoka, mlipo na mnapokwenda.
“Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la 2022 katika Ibara ya 72 (1) inatambua kuwa Mkutano Mkuu ni kikao kikubwa cha Chama katika ngazi ya wilaya, aidha Ibara ya 74 imetamka kazi za msingi za Mkutano huu kuwa ni kuzungumza mambo yote yanayohusu ulinzi na usalama na maendeleo kwa ujumla katika wilaya,” amesema.
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM Bukombe amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizosaidia utekelezaji wa idadi kubwa ya miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo.
“Nyie wenyewe mmeona yaliyofanyika Bukombe ni mengi sana na hakuna mkoa wilaya au jimbo ambalo halikuguswa na Rais Samia.
“Hii ndio sababu ya msingi  iliyofanya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika Dodoma Januari mwaka huu  kumchagua kuwa mgombea wa chama chetu kwa nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025,” amesema.
Pia amewaambia wana Jimbo kuwa hawakufanya makosa kumpa kura Dotto Biteko kwa kuwa mambo mazuri yasingetokea kama wasingemchagua.
Kikwete amewataka wananchi wa Bukombe kuwachagua wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ili kuendeleza miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo.
Naye Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.
“ Nianze kwa kusema kwa yote yaliyotekelezwa katika Jimbo hili yametokea  kwa sababu ya matashi mema ya Rais Samia Suluhu Hassan, anatupenda  sana wananchi wa Bukombe, kwa kipindi ambacho nimekuwa mbunge nimeona  ametoa fedha nyingi  sana kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Jimbo leo,” amesema.
Vilevile, amesema Rais Samia ameridhia ujenzi wa barabara ya kutoka Ushirombo hadi Katoro kwa kiwango cha lami na kuwa mkandarasi anatafutwa kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amempongeza Kikwete kwa  jitihada alizofanya wakati wa uongozi wake kwa kujenga msingi mzuri wa kuhakikisha watoto wanapata elimu nchini.

You Might Also Like

Makamanda Wa Polisi Msiende Nyumbani na Vyeo Vya Ukamanda

Watanzania Washauriwa Kula Senene, Kumbikumbi, Msusa, Ngogwe Kuepuka Udumavu

Watafiti Wa Mimea Vamizi Watua Serengeti

Ridhiwani, Ulega Washiriki Maulid Ya Kumswalia Mtume Muhammad

Kamati Ya Bunge Ya Ustawi Na Maendeleo ya Jamii, Yaipongeza Serikali Uwekezaji Kiwanda Cha Chai

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ruto: Diplomasia Itumike Kumaliza Mgogoro Kongo
Next Article Kanisa CAG Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?