MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Katoro Yapata Gari Jipya la Zimamoto, Kuwasili Februari 9
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Katoro Yapata Gari Jipya la Zimamoto, Kuwasili Februari 9
Habari

Katoro Yapata Gari Jipya la Zimamoto, Kuwasili Februari 9

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Katoro mkoani Geita, Kija Ntemi amehoji Serikali kuhusu upatikanaji wa huduma za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika jimbo hilo, akitaka ufafanuzi wa lini eneo hilo litapatiwa gari la zimamoto ili kuboresha huduma za dharura.
Ntemi amewasilisha swali hilo bungeni jijini Dodoma, akieleza kuwa ukosefu wa gari la zimamoto umekuwa changamoto kubwa kwa wananchi wa Katoro pindi majanga ya moto na dharura nyingine yanapotokea.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohamed Mahmoud, amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuliimarisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao.
Amesema Serikali imekuwa ikiipa kipaumbele sekta hiyo kwa kuimarisha vitendea kazi, ikiwemo ununuzi wa magari ya kisasa ya kuzima moto na uokoaji, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa jeshi hilo kuwafikia wananchi kwa wakati na kutoa huduma kwa ufanisi.
Naibu Waziri amefafanua kuwa Jimbo la Katoro tayari limepatiwa gari moja jipya la zimamoto na uokoaji aina ya IVECO, ambalo ni la kisasa na linatarajiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma za zimamoto katika jimbo hilo na maeneo ya jirani.
Aliongeza kuwa kwa sasa gari hilo lipo mkoani Dar es Salaam likikamilishiwa taratibu za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Geita.
Kwa mujibu wa ratiba, gari hilo linatarajiwa kuwasili Geita Februari 9, 2026.
Naibu Waziri alisema ujio wa gari hilo utaimarisha usalama wa wananchi wa Katoro kwa kusaidia kukabiliana kwa haraka na majanga ya moto pamoja na dharura nyingine, hivyo kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

You Might Also Like

Wananchi wahamasishwa kuandika historia mpya kupitia kura

Serikali Kuendelea Kuboresha Sheria za Ulinzi wa Watoto

Majaliwa  awataka waandamizi, vyombo vya usalama kutekeleza 4R

Dkt. Biteko ashiriki kilele cha miaka 60 JWTZ

TEA Yakabidhi Miradi Iliyokamilika Wilayani Mtama, Masasi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Waziri Mbarawa Aagiza Adhabu Kali kwa Madereva, Makondakta Wanaonyanyasa Wanafunzi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mbarawa Aagiza Adhabu Kali kwa Madereva, Makondakta Wanaonyanyasa Wanafunzi
Habari February 4, 2026
Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?