MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kapinga : Bei ya umeme Tanzania ni nafuu kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Kapinga : Bei ya umeme Tanzania ni nafuu kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki
Uncategorized

Kapinga : Bei ya umeme Tanzania ni nafuu kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
2 Min Read

Na Mwandishi wetu

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema gharama ya kununua umeme nchini ipo chini ukilinganisha na Nchi nyingine za Afrika Mashariki ni kutokana na Serikali kuweka ruzuku kwenye gharama ya mwananchi kununua umeme.

Kapinga amesema hayo leo Agosti 30, 2024 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya Wabunge ambao walitaka kufahamu iwapo kuanza kwa uzalishaji umeme katika mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) kutapunguza gharama ya ununuzi wa umeme na lini Serikali itashusha bei ya umeme.

“Mheshimiwa Spika, bei ya sasa ya umeme tayari ina ruzuku za Serikali ndani yake ambapo kwa sasa wastani wa bei ya uniti 1 ya umeme yenye ruzuku ni shilingi 100 kwa matumizi ya kawaida chini ya uniti 75 kwa mwezi na bila ruzuku inakuwa shilingi 292.” Amefafanua Kapinga.

Ameongeza kuwa, kwa mwananchi anayetumia zaidi ya uniti 75 kwa mwezi, analipa kiasi cha shilingi 292 kwa uniti 1 ya umeme yenye ruzuku badala ya shilingi 320 bila ruzuku.

Kuhusiana na suala la kupunguza bei ya uniti za umeme, Kapinga amesema Serikali itaendelea kufanya tathmini ya gharama za utoaji wa huduma za TANESCO mara kwa mara na kuendelea kurekebisha bei kulingana na gharama za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme utakavyokuwa.

Akijibu swali kuhusu mradi wa upelekaji wa umeme kwenye maeneo ya migodi iliyopo Chunya, mkoani Mbeya,Kapinga amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi ili akamilishe mradi huo mapema.

Kuhusu ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Hanang mkoani Manyara amesema ujenzi wake utatekelezwa katika mradi wa gridi imara Awamu ya Pili.

Akizungumzia upelekaji umeme wa gridi kwenye maeneo ya Visiwa, Kapinga amesema Tanzania ina visiwa takriban 120 na Serikali imeanza kufanya tathmini ya kufikisha umeme wa gridi katika maeneo hayo.

Ameongeza kuwa, kwa sasa visiwa hivyo vinatumia umeme wa jua ambapo Serika imeweka ruzuku ya asilimia 50 hadi 55 ili wananchi wapate umeme wa uhakika kwa muda wote.

You Might Also Like

Rais Mwinyi aipongeza Airpay kudhamini tamasha la fahari ya Zanzibar, kusaidia wananchi kupata mikopo kidigitali

Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi,waweke pingamizi

Samia Kalamu Award yasogeza Mbele

Bandari ya Kilwa kuleta mapinduzi sekta ya uvuvi nchini

Waziri Jenista akabidhiwa ofisi rasmi na Ummy Mwalimu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Majaliwa ataka kuondolewe vikwazo vya rufaa za matibabu Afrika Mashariki
Next Article Watakiwa kufanya utafiti kubaini chanzo cha makosa ya walimu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?