MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kamishna TFS Aongoza Kikao Cha Viongozi Wa Kamisheni ya Misitu Afrika
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kamishna TFS Aongoza Kikao Cha Viongozi Wa Kamisheni ya Misitu Afrika
Habari

Kamishna TFS Aongoza Kikao Cha Viongozi Wa Kamisheni ya Misitu Afrika

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na Mwandishi Wetu, Accra

KAMISHNA wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, ameongoza kikao cha Baraza la Uongozi la Kamisheni ya Misitu na Wanyamapori Barani Afrika (African Forestry and Wildlife Commission – AFWC) kinachofanyika kwa siku tatu jijini Accra, Ghana.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi waandamizi kutoka nchi wanachama wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa lengo la kujadili maendeleo, changamoto na mikakati ya pamoja ya kuimarisha usimamizi endelevu wa misitu na wanyamapori barani Afrika.

Pia kinatumika kuandaa mkutano wa 25 wa Kamisheni hiyo, unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu Pamoja na maadhimisho ya Wiki ya Misitu na Wanyamapori Afrika.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao  hicho, Profesa Silayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Misitu (Committee on Forestry – COFO) amesema Kamisheni hiyo ni jukwaa muhimu kwa nchi za Afrika kujadili sera, mafanikio na changamoto zinazokabili sekta ya misitu na wanyamapori.

Amesisitiza kuwa AFWC pia ina jukumu la kushauri FAO na nchi wanachama kuhusu sera, mipango na mbinu bora za usimamizi wa rasilimali hizo kwa kuzingatia mahitaji ya kikanda.

Ameongeza kuwa Kamisheni hiyo huchochea ushirikiano wa kikanda baina ya nchi za Afrika katika nyanja za uhifadhi na matumizi endelevu ya misitu na wanyamapori, na hufuatilia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kama vile Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC), Mkataba wa Bioanuwai (CBD), na Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa (REDD+).

Aidha, Kamisheni huwasilisha msimamo wa pamoja wa Afrika katika maamuzi ya Kamati ya Kimataifa ya Misitu (COFO).

Profesa Silayo amebainisha kuwa kikao hicho ni fursa adhimu kwa bara la Afrika kufanya tathmini ya utekelezaji wa sera mbalimbali na kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda kwa manufaa ya sasa na ya vizazi vijavyo.

Amesisitiza kuwa katika kipindi hiki cha changamoto za kimazingira, ongezeko la watu na shinikizo kwa rasilimali asilia, bara la Afrika linahitaji kuwa na msimamo mmoja na hatua madhubuti za pamoja.

Miongoni mwa viongozi walioungana na Profesa Silayo katika kikao hicho ni Abbey Haile Gabriel, Mkurugenzi Msaidizi wa FAO Kanda ya Afrika; Pierre Taty, Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Misitu (COFO); Profesa Labode Popoola, Katibu Mtendaji wa Jukwaa la Misitu Afrika (AFF); na Edward Kilawe, Katibu wa Kamisheni ya Misitu na Wanyamapori Afrika.

Kamisheni ya Misitu na Wanyamapori Afrika (AFWC) ni chombo cha kikanda kilichoanzishwa chini ya FAO kwa madhumuni ya kuratibu, kushauri na kuendeleza usimamizi endelevu wa misitu na wanyamapori katika bara la Afrika.

Makao yake makuu yapo katika Ofisi za FAO Kanda ya Afrika jijini Accra, Ghana. Kwa sasa, Kamisheni hiyo inaongozwa na Tanzania kupitia Profesa Silayo, hatua inayoakisi mchango mkubwa wa nchi katika majukwaa ya kimataifa ya uhifadhi wa mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu

You Might Also Like

Shirikianeni kutekeleza majukumu- Possi

Rais Samia Awakumbuka Wazazi Wanaojifungua Watoto Njiti

Kanisa CAG Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025

Tanzania Ipo Tayari Soko la Pamoja kuuziana Umeme – Biteko

Polisi wazuia uhalifu Tanganyika Packers

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Taasisi Za Serikali Zapewa Wiki Tano Kujiunga Na Mfumo
Next Article UDSM Chasaini Mikataba Na Kampuni Za Kichina, Kujengea Uzoefu Wanafunzi Wake
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mchumi Ajitosa Kuwania Ubunge Manyoni
Habari July 1, 2025
Msomi Wa Afya, Fatuma Atia Nia Jimbo la Dodoma Mjini
Habari July 1, 2025
Dkt. Mashimba Achukua Fomu Ya Kuwania Nafasi Ya Ubunge
Habari July 1, 2025
TPHPA, MUCE Wasaini Hati Ya Makubaliano Maeneo Yanayogusa Sayansi
Habari July 1, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?