MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kamati Ya Bunge Yaridhishwa Na Utaratibu Wa Manunuzi Ya Bando
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kamati Ya Bunge Yaridhishwa Na Utaratibu Wa Manunuzi Ya Bando
Habari

Kamati Ya Bunge Yaridhishwa Na Utaratibu Wa Manunuzi Ya Bando

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, imeridhishwa na utaratibu wa manunuzi ya bando la tozo kwa matumizi ya Daraja la Nyerere, Kigamboni ambapo imewataka watumiaji wa daraja hilo kulipia bando kwa sababu ni nafuu, rahisi na linapunguza msongamano na kuongeza mapato.

Akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya kamati hiyo,  ilipotembelea miradi ya  Shirika la Taifa  Hifadhi  ya Jamii (NSSF) ukiwemo wa Daraja la Nyerere, Mwenyekiti wa Kamati hiyo,  Fatma Toufiq, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na NSSF katika Daraja hilo hususan ya kuweka matumizi ya bando.

“Tunaendelea kuipongeza Serikali na wenzetu wa NSSF kwa kazi nzuri sana ambayo imefanyika pale Daraja la Nyerere kiukweli kumewekwa mifumo mizuri ambayo licha ya kupunguza changamoto ya foleni lakini pia inapunguza mianya ya upotevu wa mapato,” amesema  Fatma.

Amesema Kamati pia inamshukuru Rais  Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoleta maendeleo nchini kwa manufaa ya wananchi na kuwa wanaunga mkono juhudi zote zinazofanywa na Serikali  kuwa wanaamini Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ukiwemo wa NSSF utaendelea kuleta tija kwa wanachama kupitia uwekezaji unaofanywa na Mifuko hiyo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo  Katani Katani amepongeza mfumo wa manunuzi ya bando katika Daraja hilo na kuwataka wananchi kujiunga kwani ni mfumo rahisi na rafiki na pia unaondoa foleni.

Naye,  Mariam Kisangi amesema mradi wa Daraja la Nyerere umechochea maendeleo ya wananchi wa Kigamboni, ambapo amewataka kuendelea kulipia tozo za kupita kwa kutumia bando kwani inapunguza usumbufu.

Kwa upande wake,  Athumani Maige amewataka wananchi kuendelea kutumia matumizi ya bando wakati wanapopita katika Daraja hilo na pia ameipongeza NSSF kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesisitiza elimu iendelee kutolewa kwa wananchi na watumiaji wa Daraja kutumia malipo ya bando kwani ni rahisi na inapunguza usumbufu.

“Matumizi ya bando ni mazuri na yataongeza mapato, kupunguza kero kwa watumiaji wa Daraja hivyo ni muhimu wananchi kupewa elimu zaidi ili watumie bando kuondoa usumbufu,” amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,  Masha Mshomba amesema wanaendelea kuwahamasisha watumiaji wa Daraja kulipia bando la siku, wiki au mwezi ili waweze kupita kwa urahisi hasa ukizingatia kuwa matumizi ya bando ni nafuu zaidi.

Mshomba ameipongeza kamati hiyo na kuahidi kuwa maoni, maelekezo na ushauri uliotolewa na wajumbe wa kamati hiyo wataufanyia kazi kwa ajili ya utekelezaji.

You Might Also Like

Chalamila Akagua Miradi Jimbo La Kibamba Ubungo DSM

Serikali Yapambana Kutokomeza Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele

Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata Waaswa kuwa wabunifu

Gridi Ya Taifa Ni Dhaifu Kwa Mikoa Ya Kaskazini-Mramba

Wanafunzi Kutoka Veta Kushiriki Mafunzo Japan

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mpogolo Aipongeza Halmashauri Maandalizi Mikopo Asilimia 10
Next Article Kamati Ya Bunge Yaipongeza TVLA Uzalishaji wa chanjo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
PURA Yajipanga Gesi Asilia Itumike Kwenye Magari
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?