Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MENEJA Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo amesema uchakachuaji wa mafuta unaofanyika siku hizi ni ule wa kuchanganya mafuta ambayo hayajalipiwa kodi na yale yaliyolipiwa kodi.
Kaguo amesema hayo wakati wa Mafunzo ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji kwa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA).
“Uchakachuaji wa mafuta zamani ulikuwa asilimia 80, lakini sasa Tuna asilimia nne, hiyo asilimia nne ni nini?
” Sio uchakachuaji wa kuchanganya dizeli na mafuta ya taa, sasa hivi kunakuchakachua kuchanganya mafuta ambayo hayahalipiwa kodi na yale yaliyolipiwa kodi.
“Kwa hiyo kwenye ubora haisumbui sana ila sasa tunafukuzana ili serikali ipate mapato yake,” amesema.

Amesema mwaka 2010 ilianzishwa programu ya kuweka vinasaba kwenye mafuta ambayo kwa macho huwezi kutambua kama yamewekwa.
Amesem mfumo huo ulichangia ubora wa mafuta na ulipaji kodi unaostahili.
