MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Jaffo :Wafanyabiashara Tanzania, Iran watakiwa kushirikiana kwa pamoja katika Biashara, Uwekezaji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Jaffo :Wafanyabiashara Tanzania, Iran watakiwa kushirikiana kwa pamoja katika Biashara, Uwekezaji
Uncategorized

Jaffo :Wafanyabiashara Tanzania, Iran watakiwa kushirikiana kwa pamoja katika Biashara, Uwekezaji

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
5 Min Read


Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt.Suleiman Jaffo amewataka wafanyabiashara kutoka Tanzania na Iran kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja ili kupata manufaa makubwa katika masuala ya Biashara na uwekezaji.

Ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Iran ambalo limelenga kutengeneza mashirikiano katika sekta mbalimbali sambamba na kutafuta masoko na elimu.

Dkt. Jaffo amesema wafanyabiashara hao wakishirikiana kwa pamoja nchi hizo zitakuwa na maendeleo makubwa katika upande wa kiuchumi licha ya kuwa na historia ya muda mrefu ya mahusiano ya kidemokrasia .

“Miongoni mwa jambo linalofanyika kwa Sasa ni kuwa na Jukwaa kama hili ambalo tutaweza kubadilishana mawazo wafanyabiashara na watumishi wa Serikali na hatimaye nchi hizi mbili zinakuwa na maendeleo ya kiuchumi “amesema

Amesema nchi ya Tanzania inauwanda mkubwa wa rasilimali katika ardhi, utalii, madini na gesi hivyo kupitia Jukwaa hilo litaweza kutoa fursa ya wafanyabiashara wa Tanzania na Iran kubadilishana mawazo na kuona sehemu gani kuna fursa hili waweze kuzitumia.

 

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ya kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara..kama mnavyofahamu kwamba kupitia Kituo Cha uwekezaji Tanzania (TIC) mtu anaweza kufanya usajili wa uwekezaji moja kwa moja lakini sio hivyo tu kwamba uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya sekta ya gesi, Barabara, reli hii inawawezesha wafanyabiashara wengi mbalimbali waweze kufika Tanzania na kupunguza gharama za uzalishaji katika nchi yetu”amesema Jaffo

Ameendelea kueleza kuwa hivyo jukumu la Serikali kuhakikisha inawahakikishia wawekezaji wote na wafanyabiashara kwamba Tanzania Iko mbele kabisa kuhakikisha kwamba inaweka mazingira wezeshi na kusaidia wawekezaji wote kwa kuhakikisha wanafanya uwekezaji mkubwa na wafanyabiashara huku lengo likiwa kuongeza uhalali wa kibiashara katika nchi ya Tanzania.

Aidha amesema kwa upande wa mifugo
Tanzania inabahati kubwa ya kuwa wanyama wengi hasa katika upande wa ngombe, mbuzi na kondoo hivyo hiyo
fursa kubwa kwa watanzania kupanua upande wa soko hilo katika nchi mbalimbali.

“Natoa wito kwa Watanzania na wafanyabiashara wote kuchangamkia fursa hiyo na kuhakikisha mifugo wanaifuga katika mikoa mbalimbali,”amesema na kuongeza

“Kinachotakiwa kwa sasa tuweke utaratibu mzuri wa kufanya biashara kwa lengo kubwa la kwamba mifugo hii iweze kuleta thamani kwa wananchi na kufanya biashara katika nchi ya Iran”amesema

Aidha amesema hivi karibuni Rais Dkt Samia alianzisha Tume maalumu ya Rais kwa ajili ya kushughulikia masuala ya Kodi za ndani na nje na kueleza hiyo inakwenda kutoa majawabu ya uwekezaji wa aina mbalimbali ya kibiashara katika nchi Tanzania.

“Kwahiyo ndo maana nasema tunawakaribisha wawekezaji wote na wafanyabiashara waje kushiriki na watanzania katika eneo hili…kwa sababu hivi sasa Tanzania imetegeneza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na hasa dhamira ya Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha nchi hii inashirikiana na nchi nyingine na wadau wengine katika kukuza biashara baina ya nchi hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya wafanyabiashara, wenye Kilimo, Viwanda pamoja na Biashara (TCCIA) Oscar Kissanga amesema Jukwaa hilo
limewakutanisha wafanyabiashara kutoka katika sekta mbalimbali ya ikiwemo Kilimo, Madini, Mifugo ili waweze kukutana na wafanyabiashara kutoka nchini Iran.

“Lengo la Jukwaa hili ni kutengeneza mashirikiano katika sekta hizo sambamba na kutafuta masoko na elimu…wezentu Iran wanateknolojia ya hali ya juu hivyo kupitia Jukwaa hili wataweza kubadilishana uzoefu katika kutumia biashara kama nguzo ya kuwakutanisha pamoja”amesema Kissanga

Kissanga amesema kazi kubwa ya TCCIA ni kuwauganisha na kuwatafuta wafanyabiashara kutoka katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara

“Sisi TCCIA ndio tunatoa cheti cha uhalisia unapotaka kusafirishia bidhaa zako zote nje mfano parachichi, madini ni lazima upate cheti cha uhalisia kutoka kwetu..hivyo kupitia Jukwaa hili wafanyabiashara watapata elimu juu ya umuhimu wa cheti cha uhalisia pale wanaposafirisha bidhaa zao ,”amesema.

Naye Balozi wa Iran nchini Tanzania,Hossein Alvandi amesema kupitia jukwaa hilo wataweza kuwekeza katika sekta ya Kilimo,Madini na Ufugaji.

Amesema Tanzania ni miongoni mwa eneo zuri la uwekezaji na maendeleo katika Afrika Mashariki na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC.

“Hii ni nafasi nzuri kwa uwekezaji wa ndani na wa nje hivyo kupitia jukwaa hilo ni eneo zuri la kujenga mtandao wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili,”amesema

You Might Also Like

Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam

Tanzania yang’ara miradi ya Kinywe

Mbunge Wa Kibamba Mtemvu. Ajitokeza Kujiandikisha, Kuboresha Taarifa Zake

Dkt Biteko Ahimiza Watanzania Kupiga Kura Novemba 27,2024

Wananchi Wachagua Viongozi Serikali Za Mitaa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia Akabidhi Tuzo Kwa NSSF Ya Usimamizi,  Uratibu Wa Hifadhi Ya Jamii Kw Sekta Binafsi
Next Article Watu Milioni 300 Afrika Kutumia Nishati Ya Umeme Ifikapi 2030-Biteko
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?