Na Mwandishi Wetu
GEITA MJINI: MGOMEA urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim amesema hatima ya maisha ya Mtanzania iko mikononi mwake.
Hivyo ni kuchagua maisha yabadilike kiuchumi na kijamii au kuacha yaendelee yalivyo.

Mwalim ameyasema hayo Geita Mjini akiwaomba wananchi wakichague chama hicho.
Amesema Geita kama ilivyo mikoa mingine yenye dhahabu nyingi, lakini haina kielelezo chochote cha kuonyesha alama ya madini hayo.
“Ninawaomba sana, hatima ya maisha yetu ni Oktoba 29 mwaka huu, nendeni mkaichague CHAUMMA iweze kuimarisha hali nzuri za maisha yenu.”
“Maana kama mna dhahabu na samaki wengi lakini hamna viwanda vya kuchakata haina maana,” amesema.
Amesema yupo tayari kupambana na umaskini wa Watanzania, ikiwemo kuandika Katiba Mpya.