Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WAFANYABIASHARA 366 wenye madeni ya kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 350 katika Soko la Kariakoo wameagizwa kuyalipa kabla ya kurejea sokoni hapo Februari mwaka huu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Masoko Ya Kariakoo, Hawa Ghasia amesema leo Januari 29 alipozungunza na waandishi wa habari kuhusu hatua zinazoendelea kwenye maandalizi ya kurejesha shughuli za biashara kwenye soko la Kariakoo.
Ghasia amesema hivi sasa menejimenti inaratibu kazi ya kutangaza majina ya waliokuwa wafanyabiashara kwenye soko hilo ambao wamekidhi vigezo na sifa za kurejeshwa baada ya uhakiki.
“Uhakikiuliofanywa umebaini jumla ya wafanyabiashara 1520 wanaotarajiwa kurejeshwa sokoni. Majina na fomu ya kujiunga vitatangazwa kwa umma kupitia vyombo vya habari ikiwemo tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariako na tovuti ya OR – Tamisemi,” amesema.