MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: FCC Yatatua Kero 63  Za Walaji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > FCC Yatatua Kero 63  Za Walaji
Habari

FCC Yatatua Kero 63  Za Walaji

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
TUME ya Ushindani (FCC),   imesema  katika kipindi cha robo  mwaka    imeatua malalamiko 63 yaliyowasilishwa ambapo malalamiko 45 yamepatiwa ufumbuzi huku malalamiko 19 yakiwa katika hatua mbalimbali za utatuzi.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa FCC,Khadija Ngasongwa amesema hayo wakati akielezea mafanikio ya Tume hiyo na kuongea kuwa pamoja na kushughulikia malalamiko, Tume hiyo pia ina jukumu la kusajili mikataba mbalimbali kwa mujibu wa sheria.
Amesema   mikataba hiyo hupitiwa ili kuhakikisha inazingatia taratibu na kulinda maslahi ya walaji pamoja na sekta ya kifedha.
‎Aidha, amebainisha kuwa taasisi za fedha hasa katika sekta ya mikopo ya kifedha haziruhusiwi kuongeza riba au kufanya mabadiliko katika programu zao bila kupitia Tume ya Ushindani kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
Habari Picha 11322
Pia ameongeza kuwa Tume ya Ushindani imekuwa ikifanya ushirikiano mkubwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kujadili namna ya kuwalinda walaji hasa katika sekta za kifedha ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi.
‎Amesema kuwa ushirikiano huo umefanyika kwa lengo la kuboresha huduma jumuishi za kifedha kupitia mifumo madhubuti ya kushughulikia malalamiko ya wateja ili kuhakikisha wanapata huduma bora.
‎Aidha amebainisha kuwa katika kuboresha huduma kwa wananchi, Tume imefanya ushirikiano na Wakala wa Vipimo pamoja na wadau wengine kufuatilia malalamiko ya watumiaji wa huduma za intaneti ambapo wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia matumizi ya vifurushi vya data.
‎Amesema kuwa tafiti zinafanyika ili kuhakikisha wananchi wanapata thamani halisi ya fedha wanazolipia kulingana na huduma wanazotarajia.
‎Pia ameongeza kuwa hatua hizo zinalenga kusaidia kukuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha ushindani huru na wezeshi unaimarika pamoja na kuimarisha uchumi wa soko.
‎Aidha amebainisha kuwa katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2050, Tume inalenga kuhakikisha ushindani wa kibiashara unaimarika ili kuongeza nguvu ya ununuzi kwa wananchi na kuchochea mzunguko sahihi wa fedha katika uchumi.
Pia amebainisha kuwa Tume itaandaa vikao vya uelimishaji vitakavyowahusisha wazalishaji, walaji na Serikali kwa lengo la kujadili masuala muhimu yatakayosaidia kuboresha sekta hizo.
‎Amesema kuwa kupitia majadiliano hayo, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara huku walaji wakipata huduma bora zaidi.
‎Aidha ameongeza kuwa Tume inaendelea kutekeleza miradi ya kidigitali kwa ajili ya kuboresha huduma zake kupitia mfumo wa Automation of Business Process.
Pia amebainisha kuwa katika kutekeleza mradi huo, Tume imeingia ubia na taasisi ya Trade Mark Africa ambapo kiasi cha dola za Marekani laki sita, sawa na takribani sh bilioni 1.4 kimetengwa kwa ajili ya kuboresha mifumo ya huduma pamoja na kuimarisha udhibiti wa bidhaa bandia nchini.

You Might Also Like

Rais Samia na maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ

TUCTA Yafuatilia Hotuba Ya Waziri Mkuu Bungeni

Silaa: Akili Mnemba, Roboti kuongeza ufanisi,ubunifu 

ICGLR Yajipanga Kujiimarisha Amani Katika Kanda

CHAUMMA kuanzisha mjadala wa elimu ndani ya siku 100

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tembo Wasaidia Kueneza, Kuotesha Mimea Asilia
Next Article Mifugo Mingi Chanzo Cha Uchafuzi Maji Ziwa Victoria
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TASFAM Yawawezesha Wanawake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kuadhimisha Siku ya Mwanamke
Habari March 9, 2026
Nyamhokya Atoa Wito kwa Wanawake Kusimama Imara Kiuchumi
Habari March 7, 2026
Balozi Seokolo Atoa Wito Kuimarisha Biashara na Viwanda Kanda ya SADC
Habari March 7, 2026
Mkunda: Wanawake Wapewe Nafasi Katika Uongozi wa Vyama vya Wafanyakazi
Habari March 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?