Na Danson Kaijage
DODOMA: MAMLAKA ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imefanikiwa kudhibiti ujangili wa wanyama pori na kusababisha kuongezeka kwa asilimia 40 ya faru weusi katika hifadhi hiyo.
Hayo yameelezwa na Kamishina wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro ,Dkt. Elirehema Doriye wakati wa kutoa taarifa ya maendeleo kwa miaka minne ya utawala wa Serikali iliyopo madarakani katika ukumbi wa mikutana wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.

Amesema mbali na faru weusi kuongezeka kwa sasa hata simba wameongezeka na kufikia 188 kwenye hifadhi hiyo na tembo kuongezeka kutoka 800 hadi 1300.
Akizungumzia mafanikio katika sekta utalii amesema kuwa hifadhi ya Ngorongoro ni maeneo yanayotembelewa na watalii wengi nchini kutokana na vivutio vyake kuwa ni vya kipekee.
Anasena kuwa takwimu zinaonesha kati ya Julai 2021 hadi Februari 2025 jumla ya watalii 2,916,540 wametembelea vivutio vya utalii ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Dk.Doriye amesema katika kipindi kama hicho mapato ya Sh. Bilioni 693.9 yamekusanywa na kuingia kwenye mfuko mkuu wa Serikali