MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Epukeni Mikopo Inayowafilisi,Tumieni Taasisi Zinazotambulika Na BOT – Mkuu Wa Wilaya Komba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Epukeni Mikopo Inayowafilisi,Tumieni Taasisi Zinazotambulika Na BOT – Mkuu Wa Wilaya Komba
Habari

Epukeni Mikopo Inayowafilisi,Tumieni Taasisi Zinazotambulika Na BOT – Mkuu Wa Wilaya Komba

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
GEITA: MKUU wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kutumia taasisi za kifedha zilizosajiliwa na kutambuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ili kuepuka kupoteza fedha na mali kwa taasisi za kifedha zisizo rasmi.
Komba amesema hayo alipotembelea banda la Benki Kuu Tanzania katika maonyesho ya sekta ya madini yanayoendelea mkoani Geita.
Habari Picha 9637
Amesema  matumizi ya taasisi zisizosajiliwa ni chanzo kikubwa cha malalamiko, hasara, na migogoro ya kifedha kwa wananchi.
“Natoa rai kwa wananchi kutumia taasisi zinazotambulika kisheria ili kama changamoto ikitokea, Benki Kuu na wadau wake waweze kuchukua hatua kumlinda mtumiaji,” amesema.
Ameongeza kuwa baadhi ya taasisi zisizo rasmi zimekuwa zikitumia mwanya wa kukosekana kwa usimamizi kutoa mikopo kwa riba kubwa, ambayo huishia kuwafilisi wananchi.
Habari Picha 9638
“Tumepokea malalamiko kutoka maeneo mbalimbali, hasa katika mji mdogo wa Katoro, ambako baadhi ya taasisi zisizotambulika zimekuwa zikiwatoza riba kubwa wananchi na hata kuwanyang’anya nyumba,” amesema.
Katika ziara hiyo, Komba pia ameelezwa kuridhishwa na ushirikiano kati ya DIB na BoT katika kulinda amana za wananchi wanaotumia taasisi rasmi.
“Kuweka fedha kwenye taasisi zinazotambulika kuna faida kubwa, kwani hata ikitokea changamoto, kuna bodi inayoshirikiana na BoT kuhakikisha fedha za wananchi hazipotei,” amesema..
Habari Picha 9639
Mkuu huyo wa wilaya ameonya kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya taasisi au watu binafsi wanaotoa huduma za kifedha bila usajili.
“Taasisi zinazokopesha bila usajili ni tishio. Tumechukua hatua kwa baadhi yao kwa kushirikiana na BoT kupitia kitengo chao cha uchunguzi. Tutaendelea kuwafuatilia na kuzifungia,” amesema.
Amewaonya wananchi dhidi ya tamaa ya fedha za haraka kupitia taasisi zisizojulikana, hasa zile zinazotuma ujumbe mfupi wa ofa za mikopo kwa njia ya simu.
“Kwa sasa, matapeli wanatumia teknolojia kutuma ujumbe wa mikopo ya haraka. Tuachane na tamaa hizi. Tuchague taasisi zinazotambulika ili serikali iweze kutulinda iwapo changamoto itatokea,” amesema.
Habari Picha 9640
Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuwezesha sekta binafsi, jambo lililoonekana wazi kwenye maonyesho hayo.
“Mwaka jana tulikuwa na washiriki 300. Mwaka huu wamefika zaidi ya 600. Hii ni ishara kuwa sekta binafsi inakua, na juhudi za Rais Samia zina matokeo chanya,” amesema..
Habari Picha 9641

You Might Also Like

Mjadala na Kampuni za Nishati Kimataifa Kuendelezwa

REA Yapamba Moto Uhamasishaji Matumizi Ya Umeme

TRAWU Kupambania Mkataba Wa Hali Bora Kwa Wafanyakazi

Mtego wa Inzi Wa Matunda Suluhisho Salama kwa Wakulima

Tanzania Kujifunza Teknolojia Ya Magari Ya Umeme Singapore- Biteko

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mkuu Wa Wilaya Komba Aitaka DIB Kuongeza Ulinzi Kwa Fedha Za Wananchi Katika Vikoba, SACCOS
Next Article TFS Yashiriki Maonesho ya Nane ya Madini Geita
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Madaktari Kutoka Ireland Watoa Matibabu Ya Mifupa Kwa Watoto MOI
Habari October 20, 2025
Mwalim: Nikichaguliwa urais, Kigaila atakuwa Waziri Mkuu wangu
Habari October 20, 2025
ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?