MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt.Mpango ataka Afrika kuunganisha nguvu uendelezaji wa Jotoardhi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Dkt.Mpango ataka Afrika kuunganisha nguvu uendelezaji wa Jotoardhi
Uncategorized

Dkt.Mpango ataka Afrika kuunganisha nguvu uendelezaji wa Jotoardhi

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
3 Min Read

 

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Makamu wa Rais,Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Bara la Afrika linapaswa kuunganisha nguvu na kushirikiana ili kuweza kuendeleza ipasavyo nishati ya Jotoardhi ambayo ni safi na endelevu na kuondokana na nishati zisizo safi katika kuzalisha umeme ikiwemo mafuta mazito.

Dkt.Mpango amesema hayo jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2024 wakati akifungua Kongamano la Jotoardhi Afrika (ARGeo-C10) ambalo limehudhuriwa na washiriki 800 kutoka nchi 21 duniani.

Aidha, amesema kila nchi inapaswa kuwa na Taasisi maalum kwa ajili ya kusimamia uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi na kuwa na kanuni na sheria madhubuti zitakazowezesha sekta binafsi kushiriki katika uendelezaji wa nishati hiyo.

Vilevile ameziasa nchi zenye Nishati ya Jotoardhi kufanya mazungumzo ya kimkakati na Taasisi za kifedha ikiwemo Mabenki ili kupata fedha za kuendeleza nishati hiyo kutokana kuhitaji fedha nyingi katika uendelezaji wake badala ya kutegemea bajeti za Serikali pekee.

Amesema mipango ya Tanzania ni kuwa na umeme wa kiasi cha zaidi ya megawati 5000 ifikapo mwaka 2030 kutoka vyanzo mchanganyiko huku nishati jadidifu ikipewa kipaumbele ikiwemo Jotoardhi, upepo na Jua.

Katika kongamano hilo, Dkt. Mpango amewakaribisha Wawekezaji ili kuendeleza nishati ya Jotoardhi katika vyanzo mbalimbali ikiwemo Ngozi (70MW), Kiejo-Mbaka (60MW), Songwe (kati ya 5 na 35MW), Natron (60MW) na Ruhoi (5MW).

Pia amekaribisha washiriki wa ARGeo-C10 kufanya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya madini na kufanya utalii katika vivutio mbalimbali ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Serengeti na Ngorongoro.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Capt. George Mkuchika amesema chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan sekta ya nishati imezidi kupiga hatua ambapo umeme vijijini umefika kwa takriban asilimia 98 na ifikapo Desemba mwishoni vijiji vyote vitakuwa vimesambaziwa.

Ameeleza kuwa hali hiyo ni kielelezo cha mahitaji ya umeme kuongezeka hivyo lazima uendelezaji wa vyanzo mchanganyiko vya nishati uongezeke ikiwemo Jotoardhi ambayo ikiendelezwa itaweza kuzalisha umeme wa megawati 5000.

Naye Waziri wa Nishati na Mafuta kutoka Kenya, James Wandayi amesema kuwa nchi hiyo tayari imepata mafanikio katika nishati ya Jotoardhi kwani kwa sasa zaidi ya asilimia 45 ya umeme nchini humo unazalishwa na Jotoardhi.

Amesema Nishati ya Jotoardhi inapaswa izidi kupigiwa chapuo barani Afrika kutokana na kuwa ni endelevu ambapo licha ya kutumika kuzalisha umeme inatumika pia kwenye sekta nyingine ikiwemo kilimo na ufugaji.

Awali, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alimshukuru Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujitoa kwake katika kuendeleza Sekta ya Nishati na uongozi wake unaotoa Dira katika kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu Sekta.

Amesema Jotoardhi itawezesha azma ya Tanzania kuwa na umeme unaotokana na vyanzo mchanganyiko huku lengo likiwa ni kuzalisha kiasi cha megawati 995 kutokana na nishati hiyo ifikapo mwaka 2024 hali itakayoongeza pia usalama wa gridi ya umeme.

You Might Also Like

Bandari ya Kilwa kuleta mapinduzi sekta ya uvuvi nchini

Hakuna Vituo Bandia vya Kuandikisha Wapigakura:Mchengerwa

Profesa Kabudi Amimina Pongezi TEA

TASU yaiomba serikali inunue meli kutoa ajira kwa mabaharia

Tanzania yang’ara miradi ya Kinywe

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tanzania Kujifunza Teknolojia Ya Magari Ya Umeme Singapore- Biteko
Next Article TFS Yawataka Wananchi Kufuga Nyuki Kuzuia Uharibifu Wa Mazingira
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?