MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt. Ikomba wa CWT Aeleza Jinsi Elimu Ilivyobadilisha Taswira ya Tanzania kwa Miaka 64
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt. Ikomba wa CWT Aeleza Jinsi Elimu Ilivyobadilisha Taswira ya Tanzania kwa Miaka 64
Habari

Dkt. Ikomba wa CWT Aeleza Jinsi Elimu Ilivyobadilisha Taswira ya Tanzania kwa Miaka 64

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
KATIKA kuadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimeeleza kuwa sekta ya elimu imepitia mageuzi makubwa yaliyowezesha kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu na kuinua ubora wake.
Rais wa CWT, Dkt. Suleiman Ikomba, amesema hayo leo  Disemba tisa, 2025, akibainisha kuwa tangu enzi za Elimu ya Kujitegemea hadi mabadiliko ya sasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hatua kubwa zimepigwa.
Amesema mara baada ya Uhuru, serikali ilijikita katika kupanua shule za msingi vijijini na kuongeza uandikishaji kupitia kampeni ya Elimu ya Msingi kwa Wote.
Amesema kipaumbele kwenye kusoma, kuandika na kuhesabu kuliweka msingi thabiti kwa mfumo wa elimu uliokuwa unakua.
Amesema kuanzia  mwaka 1995 hadi 2010, utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na ule wa Sekondari (MMES) uliwezesha ujenzi na upanuzi wa shule katika kila kata, kupunguza uwiano wa mwanafunzi kwa mwalimu na kuongeza ufaulu.
“Mwaka 2015, serikali ilizindua rasmi sera ya Elimu Bila Ada, hatua iliyoleta ongezeko kubwa la wanafunzi, ujenzi wa madarasa, maabara na mabweni, pamoja na maboresho ya mitaala inayolenga ujuzi na fikra pevu,” amesema.
Kwa mujibu wa Dkt. Ikomba, miaka ya 2020 hadi 2025 imeonyesha kasi mpya kupitia elimu ya kidijitali, kuimarika kwa TEHAMA shuleni na mkazo katika ujuzi wa karne ya 21 kama ubunifu, teknolojia na stadi za maisha.
Katika ujumla wa miaka 64 ya Uhuru, Tanzania imejikita katika kudumisha amani, mshikamano na diplomasia imara, huku elimu ikiendelea kuwa injini ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kutoka falsafa ya Elimu ya Kujitegemea hadi mfumo unaoangazia ubunifu na teknolojia za kisasa.

You Might Also Like

Mwambungulu Asisitiza Ushirikiano Na Serikali

JMAT Yatoa Neno Yanayoendelea Kwa Vijana Wa Kenya

Askofu Akemea Midoli Kuvishwa Nguo Za Ndani

Wakazi Wa Ntyuka Wataka Kiongozi Mchapakazi

TIB Yaanda Mkakati Kabambe Wanawake Kuchangamkia Fursa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Profesa Ndunguru: Mtafiti Aliyejitoa Kusaidia Dunia Kupata Chakula Cha Baadae
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Profesa Ndunguru: Mtafiti Aliyejitoa Kusaidia Dunia Kupata Chakula Cha Baadae
Makala December 9, 2025
Profesa Ndunguru Abainisha Mwelekeo Mpya Wa Mageuzi Ya Kilimo Duniani
Habari December 9, 2025
TPDC na PURA Hakikisheni Watanzania Wananufaika na Rasilimali za Mafuta na Gesi- Salome
Habari December 8, 2025
Serikali Kuanzisha Kituo Maalum Cha Kuwezesha Wawekezaji Vijana
Habari December 8, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?