Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MKOA wa Dar es Salaam, unatarajia kuunda Kamati Maalum itakayofanya kazi ya kupitia majengo yote katikati ya mji ambayo yamechakaa, ya muda mrefu, na yale yasiyoakisi sura ya mji kwa sasa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema hayo Januari 30, 2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkubwa wa nishati uluomalizika hivi karibuni.
“Kwa hiyo nitapendekeza utaratibu mzuri ambao utashirikiana na wamiliki wa majengo, kuweza kupata wabia toka sekta binafsi ili kuweza kuongeza zaidi hotel, kumbi za mikutano na vitega uchumi zaidi,” amesema Chalamila.