Na Lucy Lyatuu
KAMPUNI ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) yenye lengo la kuwajenga ili kuzifikia fursa mbalimbali zilizoko kwenye miradi mikubwa ndani na nje ya nchi.
Wanafunzi waliolengwa ni wa fani ya uhandisi,sayansi na teknolojia Ili waweze kujua yanayohitajika katika kazi watakazozifanya na kuwa na tija zaidi.
Naibu Meneja wa CCCC Tanzania Liyuliang Lee amesema hayo Dar es Salaam alipokutana na wanafunzi hao kwa mara ya kwanza katika Taasisi hio Ili kutambulisha Kampuni hiyo ya kimataifa inayofanya kazi mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Lee amesema Kampuni hio ambayo inamilikiwa na serikali ya China Iko nchini Tanzania tangu 2009 na imekuwa ikijishughulisha na miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo.
Amesema Kampuni imejikita katika shughuli za ujenzi na imekuwa ikiwafikia wahitimu katika vyuo mbalimbali Ili kufundisha fursa mbalimbali zinazopatika lakini kile kinachotakiwa wanapotafuta ajira.
” Tunawafundisha Ili kuwa na tija na tunaamini kuwa baada ya miaka kadhaa wanaweza kuwa na viwango vikubwa zaidi katika kuchangia uzalishaji wa nchi na kujiongezea thamani,’ amesema Lee.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano Viwandani (DIT) Dk Sosthenes Karugaba amesema mafunzo hayo ni kuwaandaa ili kuzifikia fursa mbalimbali katika kampuni za nje.
Amesema DIT imekuwa ikiwezesha wanafunzi kupata mafunzo viwandani ambayo husaidia walengwa kufanya kazi zao Kwa ufanisi,na kuwa tayari kutumia vifaa vya kisasa.