Na Danson Kaijage
KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema Chama hicho kinatarajia kufanya mkutano Mkuu Mei 29-30 ukitangaliwa na Kamati kuu(CC) na Halmashauri kuu(NEC).
Aidha utawekwa utaratibu katika maeneo ya wazi ili wananchi waweze kufuatilia moja kwa moja mkutano huo utakapokuwa unaendelea.
na kwamba wataweka utaratibu katika maeneo ya wazi ili wananchi waweze kufuatilia moja kwa moja mkutano huo utakapokuwa unaendelea.
Makala ameeleza hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa kufanyika kwa mkutano huo ambao kwa mujibu wa Katibu ya CCM utakuwa na wajumbe halali 2000.
Amesema zitakuwepo ajenda kuu tatu, ambazo ni pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji Ilani CCM katika kipindi cha miaka mitano kwa serikali Tanzania Bara na Zanzibar.
Nyingine ni uzinduzi wa Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kuelekea 2030 itakayokuwa na mambo muhimu ambayo CCM inakwenda kuyanadi kwa wananchi .
Pia kufanya marekebisho madogo kwenye katiba ya Chama Cha Mapinduzi ambayo yatafahamika siku ya mkutano Mkuu.
Katika hatua nyingine amesema,
kutakuwa na tukio la uwekezaji jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Makao makuu ya CCM litakayofanyika Mei 28 mwaka huu.
“CCM ni chama kikubwa chenye wanachama milioni 11 jengo la makao makuu lililopo kwa sasa ni dogo hivyo halitoshi ndio mana tumeamua kujenga jengo lingine,”amesema.
Amesema mkutano Mkuu CCM unakwenda kusimamisha Taifa.