MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: BoT Yawaalika Wachimbaji Kuwekeza Serikalini, Yatoa Elimu ya Fedha
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > BoT Yawaalika Wachimbaji Kuwekeza Serikalini, Yatoa Elimu ya Fedha
Habari

BoT Yawaalika Wachimbaji Kuwekeza Serikalini, Yatoa Elimu ya Fedha

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
GEITA: BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wachimbaji wa madini, hususan wa dhahabu, kujiunga katika mfumo rasmi wa kifedha kwa kuuza dhahabu zao moja kwa moja kwa Benki Kuu ili kusaidia kukuza akiba ya fedha za kigeni na kuimarisha uchumi wa taifa.
Meneja wa Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BOT,  Victoria Msina, amesema hayo alipokuwa akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonesho ya Nane ya Madini yanayomalizika leo, Septemba 28, 2025.
Msina amesema BoT kwa sasa imejikita katika kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na wa kati, na kuwaelimisha kuhusu matumizi sahihi ya mifumo ya kifedha, ikiwemo uwekezaji katika dhamana za serikali.
Amesema Elimu hiyo inatolewa katika vituo mbalimbali vya BoT nchini pamoja na kwenye maonyesho na mikutano ya sekta ya madini.
Pia amesema katika maonesho hayo wachimbaji mbalimbali wamejitokeza katika banda la BOT kupata ufadanuzi mbalimbali.
“Tunawasihi waje tuwafundishe kwa sababu wakielewa mfumo huu, wataweza kujiinua kiuchumi na kuiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia uwekezaji wao kwenye dhamana,” amesema.
Ameongeza kwamba BoT inatoa elimu ya fedha kwa wachimbaji juu ya namna bora ya kukopa kwa malengo, matumizi sahihi ya fedha, pamoja na kutumia mifumo rasmi ya malipo inayosimamiwa na BoT. “Unakopa kwa malengo, si kwa kununua vitu visivyo na maendeleo,” amesema.
Benki Kuu ya Tanzania inatarajia kupitia ushirikiano huo, wachimbaji wa madini watachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uchumi wa taifa na kukuza ustawi wao binafsi kupitia maarifa ya kifedha.

You Might Also Like

TASU yaiomba serikali inunue kutoa ajira kwa mabaharia

Makamanda Wa Polisi Msiende Nyumbani na Vyeo Vya Ukamanda

 Rais Samia aipongeza REA

MNH Kuvuna Mifupa Kutengeneza Taya

Bodi ya mkonge kutoa ajira kwa watu 10,000 ifukapo 2030

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia Ni Mama Wa Maendeleo – Majaliwa
Next Article TBA Yakaribisha Wawekezaji Kushiriki Miradi Mikubwa ya Ujenzi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda
Habari October 17, 2025
Profesa Nombo: Ushirikiano wa VETA, Sekta Binafsi Waimarisha Mafunzo ya Ufundi Stadi
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?