MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Bodi Ya Wadhamini Ya NSSF Yaridhishwa Na Uwekezaji Wa Ubia Na Jeshi La Magereza
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Bodi Ya Wadhamini Ya NSSF Yaridhishwa Na Uwekezaji Wa Ubia Na Jeshi La Magereza
Habari

Bodi Ya Wadhamini Ya NSSF Yaridhishwa Na Uwekezaji Wa Ubia Na Jeshi La Magereza

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

Morogoro: MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kudhihirisha mafanikio ya uwekezaji wake mkubwa katika sekta ya viwanda kupitia mradi wa kimkakati wa kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichoko mkoani Morogoro.

Kiwanda hicho kimeanza rasmi uzalisha Julai mwaka jana, 2024 kimezalisha ajira kwa watanzania na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii.

Akizungumza wakati wa ziara ya Bodi ya Wadhamini ya NSSF,  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mwamini Malemi ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa kwa ubia kati ya NSSF na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri, hongereni sana. Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini tumejionea na tunathamini mnachokifanya,” amesema hayo baada ya kupokea taarifa ya Kiwanda kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Mkulazi (MHCL), Selestine Some.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema kupitia ziara hiyo ya kikazi, wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wameweza kushuhudia shughuli mbalimbali za uendeshaji wa mradi huo ulioanzishwa na Serikali kwa lengo la kupunguza nakisi ya sukari nchini.

Akisoma taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Mkulazi Some amesema katika msimu wa mwaka 2024/25, kampuni ilipanga kuzalisha tani 20,000 za sukari ya majumbani, ambapo hadi mwisho wa msimu kiasi cha tani 19,124 sawa na asilimia 96 kimezalishwa.

Amesema katika msimu wa 2025/26 kampuni itaanza pia kuzalisha sukari ya viwandani ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa kiwanda uliofanyika Agosti nane, 2024.

Some amesema uzalishaji wa sukari ya viwandani utapunguza uagizwaji wa bidhaa hiyo nje ya Nchi.

Amesema pia katika msimu wa uzalishaji wa sukari 2024/25 kiwanda kimetoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania 2,172 na zisizo za moja kwa moja 8,000, na kuongeza biashara, shughuli za kiuchumi na kipato kwa Wananchi wa Mji wa Dakawa, Dumila na vijiji jirani.

 

 

You Might Also Like

Watumishi wa Umma Watakiwa Kuwa na Nidhamu, Ubunifu

Ujenzi Miundombinu ya Kuongeza Udahili kipaumbele Cha Serikali

Rais Samia ashuhudia JOWUTA Ikiwa mwanachama wa  TUCTA 

Takukuru Kinondoni Yapokea Malalamiko 46 Kuhusu Rushwa

TSB, Wizara ya kilimo yaweka mpango wa vituo vya usindikaji mkonge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TPHPA Yaelezea Vipaumbele Vyake
Next Article Baraza La Madiwani Lampongeza Rais Samia Kwa Utekelezaji Wa Ilani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tunapokea Malalamiko Ya Wananchi, Tunayafanyia Kazi – Dario
Habari July 2, 2025
VETA Mtwara Yawafundisha Wanafunzi Uongezaji Thamani Kwenye Korosho, Mwani
Habari July 2, 2025
VETA Shinyanga Yatumia Kompyuta Kubuni Bidhaa 
Habari July 2, 2025
Wafanyakazi Wa Majumbani  700 Wapatiwa Mafunzo VETA
Habari July 2, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?