MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Bodi Ya  Bima Ya Amana Yapata Mkurugenzi  Mkuu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Bodi Ya  Bima Ya Amana Yapata Mkurugenzi  Mkuu
Habari

Bodi Ya  Bima Ya Amana Yapata Mkurugenzi  Mkuu

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

BODI  ya Wakurugenzi ya Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imemteua  Isack  Kihwili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia  Agosti mosi  mwaka huu.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Bima ya Amana,  Emmanuel Tutuba, ametangaza uteuzi huo na kusema DIB iko katika hatua za mwisho za kujitoa Benki Kuu ya Tanzania na kuwa taasisi inayojitegemea.

Uteuzi wa Kihwili ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Bodi hiyo unafuatia Serikali kuidhinisha muundo mpya wa taasisi hiyo.

“Kama sehemu ya utekelezaji wa muundo mpya ulioidhinishwa, Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Bima ya Amana imemteua  Isack  Kihwili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana kwa kipindi cha miaka mitano ijayo,” amesema Gavana Tutuba katika waraka wake kwa wafanyakazi wa DIB.

Kihwili anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa DIB.

Majukumu ya Bodi ya Bima ya Amana ni kutathmini na kukusanya michango kutoka benki na taasisi za fedha zinazopokea amana, na kusimamia Mfuko wa Bima ya Amana, kukinga amana za wateja na kulipa fidia wenye amana endapo benki au taasisi ya fedha itaanguka au kufilisika.

DIB pia ina wajibu wa kufanya ufilisi wa benki au taasisi ya fedha iliyoshindwa kuendelea na biashara ya huduma za kibenki au iliyofilisika endapo ikiteuliwa na Benki Kuu ya Tanzania kama mfilisi.

Aidha, kuanzia Julai mwaka huu, DIB imeongezewa jukumu la kushiriki katika kupunguza hasara kwa benki au taasisi ya fedha inayotetereka.

Bodi ya Bima ya Amana ilianzishwa kwa Mujibu wa Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha  ya Fedha ya mwaka 1991 na kuanza kufanya kazi mwaka 1994 kama idara ndani ya Benki Kuu ya Tanzania, ikiwa na Bodi yake ya Wakurugenzi chini ya uenyekiti wa Gavana wa Benki ya Tanzania.

DIB inaendelea kufanya shughuli zake chini ya Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kwamba sasa iko katika hatua za mwisho kuwa taasisi inayojitegemea kama ilivyo kwa taasisi kama hizi duniani kote.

You Might Also Like

Tanzania Ipo Tayari Kwa Mazungumzo Ya Urejeshwaji Malikale

Rais Samia afurahia SGR

Rais Samia Ameweka Alama Kwa Watumishi Wa Magereza Arusha,Awagawia Mitungi 528

FAJ Yataka Wahamiaji Wa Kazi Wa Afrka, Wanaokwenda Maeneo Mengine Walindwe

Waziri Mkuu Majaliwa Kuongoza Harambee Ya Mei Mosi Kitaifa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wambali: Vyama Vya Wafanyakazi Muhimili wa Uchumi, Ustawi Wa Jamii
Next Article VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?