MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Biteko – Asisitiza Umuhimu Wa Mifumo Thabiti Ya Nishati Jadidifu Kukidhi Mahitaji Ya Nishati
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Biteko – Asisitiza Umuhimu Wa Mifumo Thabiti Ya Nishati Jadidifu Kukidhi Mahitaji Ya Nishati
Habari

Biteko – Asisitiza Umuhimu Wa Mifumo Thabiti Ya Nishati Jadidifu Kukidhi Mahitaji Ya Nishati

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu ,Singapore
NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati  Dkt. Doto Biteko, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuweka mifumo thabiti ya matumizi ya Nishati Jadidifu ili kukidhi mahitaji ya Nishati kwa nyakati zote.
Dkt Biteko ameyasema hayo leo Oktoba 22, 2024 nchini Singapore wakati akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa uimarishaji wa  mifumo kwa ajili ya matumizi ya Nishati Jadidifu kwenye mkutano wa Jukwaa la Juu la viongozi wanachama wa Shirika la Kimataifa linaloshughulika na Nishati Jadidifu (IRENA) ikiwa ni sehemu ya mkutano wa kimataifa wa Wiki ya Nishati inayoendelea nchini Singapore.
Amesema sera za uwazi zitasaidia ukuaji wa sekta ya Nishati na kuvutia fursa kwa wawekezaji.
‘’Nipende kutoa witio kwa wanachama wenzangu wa IRENA kuhakikisha tunaweka sawa masuala ya kisiasa duniani, mabadiliko ya bei kwenye soko la Nishati, vita vya kibiashara, uhaba wa rasilimali kwani yana mchango mkubwa kwenye kuathiri mifumo ya usambazaji wa Nishati’.’ Amesema Dkt. Biteko
Amesema kuwa, Tanzania kupitia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa kipaumbele kwenye matumizi ya Nishati Jadidifu kwa kuwa rasilimali hiyo ipo ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya vyanzo vya umeme na kuwaalika wawekezaji  kuwekeza nchini kwenye miradi hiyo.
Awali akizungumza kwenye jukwaa hilo la IRENA, Waziri wa Utawala,Viwanda na Biashara wa Singapore Dkt. Tan See Leng amesema, nchi wanachama wameweka mikakati ya kuhakikisha wanaongeza kwa takriban asilimia 90 matumizi ya Nishati jadidifu ili kulinda usalama wa nchi zao na kupunguza gesi ya ukaa yenye athari kwa mazingira na pia kurahisisha upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia.
Ametaja masuala mengine ambayo yatapewa kipaumbele ni pamoja na kuhakikisha nchi wanachama wanaunganishwa na wanachama kwenye mifumo ya umeme ya Gridi kwa ajili ya kuuziana umeme, kuhakikisha Nishati ya umeme inapatikana kwa watu wote sambamba na kuongeza mahitaji ya umeme kwa nchi wanachama na kuimarisha mifumo na uimara wa Gridi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa IRENA,  Francesco La Camera, amesema mahitaji ya umeme yameongezeka duniani na kufikia Terabaiti 2.3, hivyo nchi wanachama  takriban 133 wanachama wa IRENA wamekubaliana kuwekeza zaidi kwenye Teknolojia, Sera na  utafutaji wa masoko na uboreshaji wa miundombinu ili kufikia lengo na tayari IRENA imetoa msaada wa kitaalamu kwa wanachama 96 kwa ajili ya kusaidia maboresho hayo.
Mjadala huo ullijadili pia masuala ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuboresha Gridi na uunganishaji wa wateja kwa nchi wanachama.
Katika Mkutano huo wa Wiki ya Nishati Singapore, Tanzania inawakilishwa na Wadau kutoka wizara ya Nishati, EWURA na TANESCO.

You Might Also Like

Mbunifu Alilia Uwepo Wa Miongozo Kwa Wagunduzi

Sheria ya ajira, mahusiano kazini ipitiwe upya

Wakulima wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea

Mbunge Kuchauka azindua kambi kuhamasisha Uchaguzi Serikali za  Mitaa

Kipanga: Lugha ya Kichina Inakuza Diplomasia, Kuimarisha Uhusiano

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mafunzo Yatolewa Katika Kongamano La Jotoardhi
Next Article Polisi Kata Kupewa Pikipiki Nchi Nzima Kuimarisha Ulinzi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?