MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Bil.19 kusambaza umeme vitongojini Tabora
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Bil.19 kusambaza umeme vitongojini Tabora
Uncategorized

Bil.19 kusambaza umeme vitongojini Tabora

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
3 Min Read

Na Mwandishi wetu.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 19 wa kusambaza umeme katika vitongoji 180 utakaonufaisha Kaya 5,940 Mkoani Tabora.

Hayo yameelezwa na Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle Novemba 07, 2024 Mkoani Tabora mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Paul Chacha wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya Sinotec kutoka nchini China.

 

“Napenda kuwafahamisha wananchi wa Tabora kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta. Samia Suluhu Hassan ameridhia kiasi cha shilingi 19,057,015,682.55 kitumike kutekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 180 mkoani hapa na leo hii tupo hapa kumtambulisha mkandarasi anayetekeleza mradi huu,” amebainisha Mhandisi Dulle.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amemuelekeza Mkandarasi kuhakikisha anakamalisha kazi hiyo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa na aliipongeza REA kwa kuendelea kutimiza dhamira ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo.

Akielezea utekelezaji wa mradi, Mhandisi Dulle amesema unatekelezwa ndani ya majimbo yote 12 ya mkoani humo na kwamba unatekelezwa kwa muda wa miaka miwili na utakamilika Mwezi Agosti, 2026 ambapo kila jimbo vitongoji 15 vitanufaika.

Amefafanua kuwa hadi sasa vitongoji vilivyosambaziwa umeme ni vitongoji 1,323 kati ya vitongoji 3,749 na kwamba vitongoji vitakavyosalia vitasambaziwa umeme kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mhandisi Dulle amesema Mradi umelenga kusogeza miundombinu ya umeme kwa wananchi katika majimbo yote ili waweze kunufaika na nishati ya umeme katika kujiletea maendeleo hasa katika kuongeza thamani ya mazao, ufundi seremala, viwanda vidogo vidogo, mashine za kusaga na kukoboa sambamba na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii.

“Vitongoji vitakavyonufaika ni kutoka katika Majimbo ya Sikonge, Urambo, Igalula, Tabora Kaskazini, kaliua, Ulyankulu, Bukene, Nzega Vijijini, Nzega Mjini, Igunga, Tabora Mjini na Manonga ambapo kila jimbo litapata vitongoji 15, Mashine umba 15 na wateja 495 na msongo mdogo (LV) umbali wa kilomita 30,” amefafanua Mhandisi Dulle.

Amesisitiza kuwa gharama ya kuunganishiwa umeme kwa wananchi ndani ya vitongoji hivyo ni shilingi 27,000 na kwamba mradi hautakuwa na fidia.

Mhandisi Dulle amesisitiza kuwa Wakala kwa kushirikiana na TANESCO unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchi nzima pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni ya kutekeleza miradi na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa ili iweze kuwanufaisha wananchi kama ilivyo dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Naye Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya Sinotec , Mhandisi Alphred Kessy alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa watakamilisha mradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

You Might Also Like

Bandari ya Kilwa kuleta mapinduzi sekta ya uvuvi nchini

Jaffo :Wafanyabiashara Tanzania, Iran watakiwa kushirikiana kwa pamoja katika Biashara, Uwekezaji

Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi,waweke pingamizi

Wananchi Wachagua Viongozi Serikali Za Mitaa

Vinasaba 524 Vimepimwa Kwa Mkemia Mkuu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Mwinyi Kuzindua Maabara Nguvu Za Atomi
Next Article Majaliwa Akazia Disemba Ni Mwisho wa Kutumia Mkaa. Gesi Kweny Taasisi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Madaktari Toka China Waleta Matumaini Barani Afrika
Makala May 16, 2025
Maziwa Kukuza Uchumi Wa Wafugaji
Habari May 16, 2025
Wizara Ya Madini Kununua Chopa, Kufanya Utafiti
Habari May 15, 2025
Serikali Kupeleka Umeme Maeneo Ya Kimkakati
Habari May 15, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?